Tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan mwezi Aprili 2023, maafisa wa eneo hilo wameripoti kuwa karibu wakimbizi 600,000 wa Sudan wamewasili kambini hapo, wengi wao baada ya safari ndefu na ngumu kupitia nchi kadhaa. Waliwasili wakiwa na mali chache, lakini wakiwa na kumbukumbu nyingi, na sasa wanajaribu kuunganisha upya maisha yao yaliyosambaratika.

Katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo takriban kilomita 275 kutoka Kampala, wanaishi wakimbizi kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Sudan, Sudan Kusini, Burundi, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Rwanda, pamoja na jamii wenyeji. Licha ya tofauti zao, wote wanaunganishwa na jambo moja kuu: uzoefu wa kupoteza na jitihada za kuanza upya.

Mtazamo wa pande zote za eneo la vijijini huko Byali, Uganda, unaonyesha barabara pana ya udongo yenye miundo ya muda pande zote mbili, miti michache, na milima katika umbali chini ya anga yenye mawingu.

UN News/Abdelmonem Makki

Takriban wakimbizi 600,000 wa Sudan wamewasili katika kambi ya Kryandungo, baadhi yao baada ya safari ndefu na ngumu wakivuka nchi nyingi.

Kwa lengo la kuona hali halisi kwa karibu, Idhaa ya Umoja wa Mataifa ilitembelea kambi hiyo kufuatilia maisha ya kila siku ya wakazi wake pamoja na changamoto wanazokumbana nazo tangu walipokimbia vita.

Kutoka kumbi za uhandisi hadi maisha ya hema

Hussein Hashim Taiman anaishi maisha ambayo hakuwahi kuyatarajia. Mhandisi wa ujenzi mwenye shahada ya uzamili, aliwahi kufanya kazi katika idara ya uhandisi wa kiraia ya ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, wa kulinda amani Darfur, Sudan, UNAMID. Leo, anaishi ndani ya hema na anaongoza jamii ya wakimbizi wa Sudan katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo, mojawapo ya kambi kubwa nchini Uganda.

Aliishi Omdurman kabla ya kulazimika kukimbia mwezi Mei 2023 akiwa na watoto wake kuelekea Sudan Kusini na baadaye Uganda, safari aliyosema ilijaa hofu, manyanyaso na mateso.

Mwanamume mwenye ndevu na nywele fupi, amevaa shati la maua, ameketi kwenye kiti cha bluu na kufanya ishara wakati akizungumza. Nyuma yake, mwanamke mwenye shati nyekundu anatembea karibu na jengo la matofali katika mazingira ya vijijini.

UN News/Abdelmonem Makki

Katika kambi ya Kryandungo, Hussein Hashim Taiman anaishi maisha ambayo hakuwahi kuwazia. Mhandisi wa ujenzi mwenye shahada ya uzamili, alikuwa akifanya kazi katika idara ya uhandisi wa ujenzi ya ujumbe wa UNAMID huko Darfur.

Anasema, “hapa unapolalamika, unagundua kuwa kuna mtu aliye na hali mbaya zaidi kuliko yako. Hivyo unajaribu kusahau maumivu yako ili kupunguza ya wengine. Tunapata nguvu kutoka kwa kila mmoja. Tulikuwa na maisha tofauti kabisa kabla ya vita; sasa ninaishi kwenye hema haya ndiyo matokeo ya vita.”

Kadri muda unavyopita, hali haijaimarika kama ilivyotarajiwa. Misaada inapungua, na mahema yaliyotarajiwa kudumu miezi sita yamekuwa makazi kwa zaidi ya miaka mitatu.

Huduma ni haba sana, huduma za afya hazitoshi, elimu si ya uhakika, na hata maji na chakula vinategemea juhudi za pamoja za wakimbizi wenyewe.

Hussein anaonya kuwa mustakabali wa kizazi kizima uko hatarini, akitoa wito kwa Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada.

Wanaume wawili wa Kiafrika wakipika nje nchini Uganda au Darfur. Mtu mmoja mwenye shati ya bluu anaketi kando ya sufuria kubwa juu ya moto wa wazi, wakati mtu mwingine mwenye shati la plaid anaangalia sufuria ya pili.

Mutasim Mohamed Ahmed

Mutasim Mohamed Ahmed Ahmed, kutoka mji wa Nyala katika jimbo la South Darfur, alikuwa akiishi Khartoum na kufanya kazi katika biashara kati ya Sudan, China, na Dubai.

Chakula kinapokuwa suala la uhai na kifo

Katika hali hii ngumu, juhudi ndogo lakini zenye athari kubwa zimeibuka. Miongoni mwazo ni majiko za kijamii, ambayo yalianza kama suluhisho la dharura lakini sasa zimekuwa tegemeo muhimu dhidi ya njaa.

Kuna takriban majiko 20 kambini, ambayo yamechangia kupunguza njaa na kuimarisha mshikamano miongoni mwa wakimbizi.

Mutasim Mohamed Ahmed, kutoka Nyala, Darfur Kusini, ambaye hapo awali alikuwa mfanyabiashara kati ya Sudan, China na Dubai, sasa ni kiongozi wa majiko hayo kambini.

Anaeleza akisema, “majiko haya yalianzishwa baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani kupunguza mgao wa chakula. Tuliona visa vya utapiamlo, vifo na hata mimba kuharibika kutokana na njaa.”

Anaongeza akisema, “kazi hii imenifundisha ubinadamu. Ukiona watu wenye njaa na uchi, lazima uwe na huruma. Hawa ni watu wangu, damu na nyama yangu.”

Mwanamume Mwafrika mwenye kanzu nyeupe na kofia anashikana mikono na wafanyakazi wawili wa kike wa misaada wakiwa wamevaa mavazi ya MDPD na hijab katika mazingira ya vijijini.

Dkt. Wadad Makki (wa pili kutoka kushoto) anasafiri umbali mrefu kufika kambi ya Kryandungo, kwa sababu amechagua kusimama na wale wanaoishi ndani kambini hiyo.

“Tuliishi… ili kuwasaidia wengine”

Kutoka Kampala, Dkt. Wadad Makki husafiri umbali mrefu mara kwa mara kwenda Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo

kusaidia wakimbizi.

Akiwa profesa wa zamani na mkurugenzi wa elimu maalum huko Khartoum, maisha yake yalibadilika kabisa kutokana na vita.

Anakumbuka na kusema,”niliondoka nyumbani wakati wa mabomu, moshi kila mahali, magari yanawaka, miili mitaani. Ilikuwa vigumu kwa watoto wangu kuona haya yote.”

Sasa anasaidia kupitia shirika la “Al-Malam Darfur for Peace and Development,” hasa kwa kusaidia katika majiko ya kijamii.

“Tulipona na kufika Uganda salama, sasa tunasaidia ndugu zetu walioko kambini.” Anasema Dkt. Makki, hata hivyo, ana hofu kuhusu muda mrefu wa vita: “Changamoto ni nyingi elimu, gharama za maisha, ukosefu wa ajira. Tunaomba vita iishe ili turudi nyumbani.”

Picha ya mtu mweusi mwenye miwani na ndevu, amevaa shati ya rangi ya kijivu yenye nembo ya 'GM', ameketi kwenye dawati la mbao katika ofisi.

UN News/Abdelmonem Makki

Dkt. Abdul Jabbar Ahmed Adam, mtaalamu wa magonjwa ya ndani, sasa anafanya kazi katika Hospitali ya Gombe mjini Kampala, Uganda.

Madaktari wakimbizi waimarisha sekta ya afya Uganda

Katika mji mkuu Kampala, baadhi ya wakimbizi wameanza kujenga upya maisha yao ya kitaaluma.

Dkt. Abdul Jabbar Ahmed Adam, daktari wa magonjwa ya ndani aliyewahi kufanya kazi Hospitali ya Ibn Sina Khartoum, sasa anafanya kazi katika Hospitali ya Gombe nchini Uganda.

Anasema: “tulipokelewa vizuri sana, hakuna ubaguzi, tunahisi kama tuko nyumbani.”

Anaeleza kuwa madaktari wengi wa Sudan wamechangia kuboresha huduma za afya nchini humo, hasa kutokana na upungufu wa wataalamu.

“Moyo Mweupe”; hadithi inayovuka vita

Ibrahim Zakaria Yahya ni mkimbizi aliyeanza maisha mapya Biale baada ya kuondoka Sudan mwaka 2007.

Baada ya miaka ya changamoto, alifanikiwa kuanzisha biashara na kufungua hoteli iitwayo “Moyo Mweupe.”

Mwanamume mwenye tabasamu, Ibrahim Zakaria Yahya, amesimama kando ya mashine ya saizi ya barafu katika duka nchini Uganda.

UN/Abdelmonem Makki

Ibrahim Zakaria Yahya anasimulia hatua za safari ndefu iliyochukua miaka mingi ya kuhama na kujaribu kupata makazi mapya.

Anaeleza maana ya jina hilo akisema, “ni mwaliko wa kusafisha mioyo na dhamiri, na kushinda machungu ya vita.”

Anasema licha ya kuwa mkimbizi, hajawahi kuhisi hivyo: “Mimi ni mkimbizi kwa jina tu,ninaishi kama raia wa kawaida hapa.”

Hata hivyo, bado anatamani kurudi Sudan siku moja

Licha ya matumaini hayo, maisha kambini bado ni magumu huduma ni chache, fursa ni haba, na hofu inaendelea hasa kwa watoto na vijana.

Hata hivyo, wakimbizi wengi wanaendelea kushikilia tumaini kwamba siku moja vita vitaisha, na watarejea nyumbani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *