Dar es Salaam. Shirika la Baba Watoto kupitia mradi wake wa Ahadi, umekabidhi kituo kwa ajili ya kutolea huduma ya afya ya uzazi kwa vijana katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana walichokiboresha kwa gharama ya Sh38 milioni.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo, Meneja mradi Kasei Msuya, lengo la kuboresha kituo hicho ni kuhakikisha wanaboresha huduma rafiki kwa vijana kwa kuondoa mazingira yaliokuwa yanawafanya wasiweze kufika au kuwaondolea uwoga.

“Lakini pia kuweza kupata huduma zinazoendana na wakati na kwa kuangalia masuala mazima ya ulinzi wao wa taarifa na usiri,”amesema.

Kituo hicho mbali ya kutoa huduma za afya, pia kina eneo rasmi kwa ajili ya mtu kujitolea kuchangia damu.

Kuhusu gharama zilizotumika kukarabati kituo hicho, amesema jumla ya Sh38.6 milioni zilitumika kati ya hizo ujenzi wa jengo pekee iligharimu zaidi ya Sh27 huku vifaa vilivyowekwa  vikigharaimu Sh12.2 milioni.

Amesema kwa ukarabati huo wanaamini idadi ya vijana watakaofika kupata huduma wataongezeka huku kwa watumishi , wataweza kutoa huduma zilizo rafiki ikiwemo kupata huduma kwa wakati.

Wakati kuhusu mradi wa Ahadi, Msuya  amesema umefadhiliwa na serikali ya Canada na unawalenga vijana wenye umri wa miaka kumi hadi 24 walioko ndani ya shule na waliopo nje ya shule

Hata hivyo amesema mradi unatendelea kukisimamia  kituo hicho kwa miezi 24 na kueleza kuwa nia yao ni kuona jengo pamoja na vifaa vikiendelea kuwa katika hali ilivyo na kuwekwa katika bajeti za hospitali na  isiwe kusubiri hadi kitu kiharibike ndio kitengenezwe.

Kwa upande wake Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi  kwa Vijana kutoka Wizara ya Afya, Gerald Kihwele,  ambaye alikuwa mgeni rasmi, amesema moja ya sababu ya kupenedekeza mradi huo ukatekelezwe  Amana ni  kutokana na mazingira ya hospitali ambayo hupokea watu wengi kutokana na kuwa katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Muonekanonwa nje wa Kituo cha kutolea huduma kwa vijana

‘Kwangu naiona ni kitu cha msingi, na tunavyoona ni kitu kinaweza kubebwa na kufanywa kwa maeneo mengine ili vijana waweze kupata huduma zilizo bora,’amesema Kihwele.

Kuhusu eneo la uchangiaji wa damu salama, amesema hilo  limekuwa wazo zuri kwa kuwa vijana watajengewa tabia ya kuchangia damu jambo ambalo pia ni la kizalendo.

“Niseme tunashukuru sana kwa kazi hii kwani imetupa imani kubwa kama serikli na kama Wizara na metufikirisha zaidi kuona namna gani tunaweza kuingalia Amana zaidi kwa jicho la kipekee ili kuweza kuboresha huduma zao,”amesema Mratibu huyo.

Awali Mkurugezi wa Shirika hilo, Mgunga Mwanyenyelwa,  aliipongeza Amana kwa kuweza kufikiwa na mradi huo, huku akiomba kuwepo kwa uendelezaji wa utoaji huduma hiyo.

“Tatizo kwetu sio uanzishaji wa mradi bali ni uendelezaji wa mradi wenyewe ukizingatia kadri miaka inavyozidi kwenda ufadhili umekuwa ni changamoto na rasilimali fedha inazidi kuwa ngumu.

“Hivyo sisi kama Baba Watoto ambao tupo huku chini , tunaguswa na watoto na vijana , tutapata nguvu ikiwa hata baada ya miaka miwili hadi mitatu, wafadhili wakija kuangalia wapaone panaendelea hata baada ya mradi kuisha kwa kuwa kumekuwa na shida katika uendelezaji wa miradi ya aina hii,”amesema Mwanyenyelwa.

Kwa upande wake Kaimu  Mganga Mfawidhi wa Amana, Dk Jumanne  Magele, amesema ni heshima kubwa kutekelezwa kwa mradi huo katika hospitali yao ukizingatia awali ulikuwa utekelezwe katika hospitali za ngazi ya chini yao.

Magele amesema kupitia mradi huo wataongeza upatikanaji wa huduma ya vijana na kupitia kituo hicho pia watatoa elimu ya umuhimu wa kuchangia damu ambayo ni zawadi kubwa kwa binadamu ukiacha uhai, elimu ya VVU, kuwapa ushauri waathirika wa ukatili wa kijinsia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *