Kasereka Nzala, ambaye ni Mganga Mkuu wa hospitali hiyo amewashukuru na kuwapongeza askari walinda amani wa JWTZ kwa msaada huo.

Mlinzi wa amani wa kike wa Tanzania, akiwa amevaa yunifomu ya kijeshi na kofia ya bluu, anampa chanjo mtoto mchanga aliyebebwa na mama yake, wakati wauguzi wawili wanapoangalia katika kliniki nchini DRC.

Kikosi cha walinda amani kutoka Tanzania TANZQRF wanaohdumu chini ya MONUSCO kinaunga mkono wahudumu wa afya na kutoa dawa na matibabu ya bure nchini DRC.

“Tunafurahi kwani MONUSCO ambao ni wa Tanzania walikuwa wakiona hilo jambo na hivi wameona ni vizuri kwa kuja kutuletea dawa na kuweza kushinda na si ndani ya kazi ya kuhudumia wagonjwa. Nafurahi kwani kwenye MONUSCO na Tanzania kuna kuna madaktari ambao tunafanya nao kazi. Kuna Madaktari, wauguzi, madaktari wa meno na wengine ambao wamesoma masomo mbalimbali ya kuhudumia wagonjwani furaha kwetu . Tulidhani wao ni askari tu lakini tumekuta ndani yao kuna madaktari ambao wanatusaidia kwa hapa kwenye hospitali ya wilaya ya Oicha na wametuletea dawa. Tunashukuru sana na Mungu aendelee kuwabariki. “

Aidha, Afisa Uhusiano wa kikundi hicho, Meja Anicet Lusozi ameeleza hatua hiyo kuwa inalenga kuendeleza na kudumisha mahusiano kati ya wananchi wa DRC na vikundi kutoka Tanzania pamoja na  vikundi vingine vya MONUSCO kwa ujumla.

“ Kikubwa zaidi ni kudumisha mahusiano kati ya jamii ya wananchi wa Congo pamoja na majeshi ya MONUSCO na Tanzania kwa ujumla. Tumekuja kukabidhi dawa za kutosha kwa watu wenye uhitaji. Tunatambua kuna wagonjwa wengi sana wanaohitaji dawa zndio maana tumeguswa. Tukaona ya kwamba tulete dawa ili zisaidie jamii ya wananchi wa Congo.”

Wanajeshi wa kudumisha amani wa Tanzania kutoka MONUSCO wanasaidia katika usajili wa wagonjwa katika kliniki ya afya nchini DRC. Mwanajeshi wa kudumisha amani mwenye kofia ya UN ya bluu na mtaalamu wa afya wameketi kwenye dawati pamoja na mgonjwa wa kike, wakiwa wamezungukwa na rafu za rekodi za matibabu.

Kikosi cha walinda amani kutoka Tanzania TANZQRF wanaohdumu chini ya MONUSCO kinaunga mkono wahudumu wa afya na kutoa dawa na matibabu ya bure nchini DRC.

Kwa upande wao raia Bw. Ezekiel Ngungu na Bi. Leticia Zangina  wamepongeza na kushukuru juhudi za walinda amani hao katika kuimarisha ulinzi na kuendeleza ushirikiano wa karibu na jamii ya eneo hilo.

“Tunashukuru sana kwa msaada wao na uwepo wao kwenye hospitali yetu na kazi zao wanazozifanya hapa kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanajitolea sana. Tunasema Mungu awabariki taifa la Tanzania na wanajeshi kwenye MONUSCO. Tunawashukuru sana. Na muendelee hii isiwe mara ya mwisho. Tunawashukuru sana. “

Kuendelea kuimarika kwa usalama Mashariki mwa DRC kunachangiwa pia na uwepo wa kikundi hiki kutoka Tanzania ambacho  kimewezesha msaada wa kibinadamu kuwafikia  wenye uhitaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *