FOUNTAIN GATE vs MTIBWA SUGAR: Kocha wa Fountain Gate, Fred Felix ‘Minziro’ amesema wanapambana kuwajenga wachezaji wa timu hiyo kisikolojia ili kuyasahau yaliyopita na kuangalia mchezo unafuata.

Minziro amesema benchi la ufundi na wachezaji wanatambua timu hiyo haipo katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa NBC Premier League, jambo linalowapa nguvu ya kupambana mpaka mwisho kuzitafuta alama tatu zitakazorejesha hali ya kujiamini kwa michezo ijayo.

Kwa upande wake mchezaji, Derick Mukombozi amesema wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila ni wajibu wao kuzipigania alama tatu na kulipa kisasi kwa Mtibwa Sugar.

Imeandikwa na Katherini Shirima
mhariri @allymufti_tz

Mchezo huo utachezwa kesho Aprili 18, na utakuwa LIVE #AzamSports1HD

#NBCPremierLeague #FountainGate #MtibwaSugar #FountainGateMtibwaSugar

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *