
Mwanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa kutoka Ufaransa ameuawa leo Jumamosi nchini Lebanon katika shamulio la kuvizia, amesema Waziri wa Ulinzi Catherine Vautrin. Sajenti Meja Florian Montorio “alikuwa kwenye misheni ya kusafisha njia hadi kituo cha UNIFIL ambacho kilitengwa kwa siku kadhaa kutokana na mapigano katika eneo hilo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mwanajeshi huyo wa Ufaransa alishambuliwa karibu sana na kundi lenye silaha. Alipigwa risasi na kufariki kutokana na majeraha baada ya wenzake kushindwa kumhudumia,” waziri huyo ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Askari mmoja wa Ufaransa ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa Jumamosi kusini mwa Lebanon wakati wa shambulio dhidi ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa, ametangaza Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, akisema kwamba “ushahidi unaonyesha kwamba Hezbollah inahusika na shambulio hili.”
“Taifa linatoa heshima na linaonyesha uungaji mkono wake kwa familia za wanajeshi wetu na wanajeshi wetu wote waliojitolea kwa amani nchini Lebanon. Ushahidi unaonyesha kwamba Hezbollah inawajibika kwa shambulio hili. Ufaransa inaomba mamlaka ya Lebanon iwakamate mara moja wale waliohusika na kuchukua majukumu yao pamoja na UNIFIL,” rais wa Ufaransa ametangaza kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Waziri mkuu wa Lebanon ametangaza siku ya Jumamosi kwamba shambulio limetokea dhidi ya walinda amani wa Ufaransa kusini mwa nchi, katika siku ya pili ya makubaliano ya amani na Israel. “Ninalaani vikali uchokozi dhidi ya wanachama wa kikosi cha Ufaransa” cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL), Nawaf Salam amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X, akiongeza kwamba ameamuru “uchunguzi wa haraka” ili kuwakamata wale waliohusika.
Msemaji wa UNIFIL amethibitisha kwa shirika la habari la AFP kwamba “tukio lilitokea” Jumamosi asubuhi huko GhandouriyĆ© kusini mwa Lebanon na kutaja kwamba uchunguzi umefunguliwa, bila maelezo zaidi kwa wakati huu kuhusu hali au waathiriwa wapya.