
Makamo wa zamani wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, anasema Rais wa sasa wa nchi hiyo Donald Trump alilazimika kuingia vitani na Iran akishirikiana na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ‘katika jaribio dhaifu la kupindisha na kupitisha mazingatio ya raia wa Marekani kutoka kwenye kesi ya Epstein.’
Akizungumza katika Ukumbi wa Huntington mjini Detroit wakati wa mkutano wa chama cha Democratic huko Michigan siku ya Jumamosi, Harris alisema, “Trump aliingia vitani, na aliburutwa na Bibi Netanyahu na lazima tukiri kwamba watu wa Marekani hawakutaka vita hivyo. Miongoni mwa matokeo mengi mabaya ya vita ni kupanda kwa bei ya mafuta.”
Akiashiria kesia ya uhalifu wa kingono ya Jeffrey Epstein, Kamala Harris amesema kwa kuanzisha mashambulizi dhidi ya Iran, Trump alitaka kubadili mwelekeo wa maoni ya umma ya Marekani kutoka kwenye ushirikiano wake na Epstein hadi kwenye vita vilivyoathiri kila kipengele cha maisha ya kila siku ya Mmarekani.
Amemlaani Trump kwa kuhatarisha uhusiano wa Marekani na washirika na kumwita “mtu asiyejiamini.”
Vilevile amemkosoa Rais Donald Trump kwa kuhatarisha uhai wa wanajeshi wa Marekani na kuchochea kile alichokiita “vita vya ndani” ambacho kinaumiza umma, huku bei za mafuta zikiendelea kuongezeka na kuathiri kaya.”Tunawajihiana na utawala wa urais wenye ufisadi, ukatili na dhaifu zaidi katika historia ya Marekani,” Harris aliongeza na kusema: Ameshindwa katika kila nyanja.”