Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Mwanamke mmoja raia wa Canada ameuawa huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya mtu aliyejihami kwa silaha kufyatua risasi katika eneo la kihistoria nchini Mexico, kwa mujibu wa maafisa wa nchi hiyo.
Tukio hilo limeibua hofu na maswali kuhusu usalama katika maeneo maarufu ya utalii.
Shambulio hilo lilitokea katika eneo la kumbukumbu ya kale la Teotihuacán lililopo kaskazini mwa Mexico City siku ya Jumatatu.
Serikali ya Mexico ilisema mshambuliaji huyo alijiua baada ya kutekeleza tukio hilo.
Polisi walipofika eneo la tukio walikuta bunduki, silaha yenye makali pamoja na risasi ambazo hazikutumika.
Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum alisema “Kilichotokea leo huko Teotihuacán kinatuumiza sana. Ninatuma salamu za pole na rambirambi kwa waathiriwa na familia zao,” aliandika kwa Kihispania.
Piramidi na magofu ya kale ya Teotihuacán ni eneo la urithi wa dunia lililotambuliwa na UNESCO, ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya watalii nchini Mexico.
Tukio hilo linaweza kuathiri taswira ya usalama katika maeneo hayo muhimu ya kihistoria.
Waziri wa mambo ya nje wa Canada Anita Anand alithibitisha kuwa raia mmoja wa Canada aliuawa na mwingine kujeruhiwa