
Chama cha TPLF ambacho kinaongoza eneo la kaskazini mwa Ethiopia, Tigray, kimetangaza kurejeshwa kwa bunge la ukanda, ambalo uchaguzi wake ulikuwa moja ya vichocheo vya vita na serikali kuu, uamuzi ambao wadadisi wa mambo wanahofia kuwa huenda ikasababisha mzozo mwingine mbaya kati ya utawala wa Addis Ababa na wapiganaj wa TPLF.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uongozi wa juu wa TPLF unasema umechukua uamuzi wa kurejesha bunge lililochagliwa mwaka 2020 katika uchaguzi ambao haukutambuliwa na serikali kuu kutokana na serikali ya Waziri mkuu Ahmed kukiuka mkataba wa amani wa Pretoria.
Ingawa serikali bado haijatoa tamko kufuatia tangazo hilo la TPLF, wadadisi wa mambo wanasema hawaoni ikiwa Addis Itakubaliana na maamuzi ya waasi hao.
Vita ya Tigray iliyoshuhudiwa kati ya mwaka 2020 hadi 2022, ilisababisha vifo vya watu zaidi ya laki 6, ambapo ilihusisha jeshi la Serikali lililosaidiwa na wapiganaji wa jadi dhidi ya waasi wa TPLF.
Tangu wakati huo, Tigray imekuwa ikitawalia chini ya mkataba wa amani wa Pretoria, ambapo mwaka jana utawala wa Addis Ababa ulitangaza kuongeza uteuzi wa viongozi wake kwa mwaka mmoja zaidi licha ya ukosoaji toka kwa TPLF.
Licha ya TPLF kuwa na ushawishi kwenye ukanda, kwa sasa sio chama cha siasa kinachotambuliwa kisheria baada ya kufutwa na utawala wa Waziri mkuu Abiy, anayedai chama hicho ni kikundi cha kigaidi na kinashirikiana na Serikali ya Eritrea, madai ambayo TPLF inakanusha.