Dar es Salaam. Mzee Steven Masatu Wassira, ndiye mtu aliyehudumu awamu zote sita. Tangu enzi za Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Jakaya, Magufuli na sasa Mama Samia. Kote huko alikuwapo na kitengo alipewa.
Nenda ‘yutyubu’ tafuta video ya Makongoro Nyerere. Akielezea uwepo wa Wasira katika awamu zote. Makongoro akiwa ni dogo sebuleni kwa Julius, alilisikia jina la Wasira kila siku akiwa waziri.
Sasa hivi kuna kiumbe kinaitwa Mose Iyobo. Huyu ndiye ‘masta’ wa mikato ya Mondi ya kucheza. Huyu ndo ‘steringi’ wa steji yote ya Mondi. Anajua na yeye anajua kuwa anajua, bodi isikuongopee.
Kifesi alimpiga picha sana Mondi akasepa, Iyobo yupo. Lukamba akaja akasepa, Iyobo yupo. Rich Mavoko kaja kasepa Iyobo yupo. Lavalava naye kaja kasepa Iyobo yupo. Mbosso kaja kasepa Iyobo yupo.
Rayvanny alimkuta Iyobo, naye kaondoka Iyobo yupo. Konde Boy alimkuta Iyobo naye alisepa zake Iyobo yupo. Mkubwa Fella naye alikuja na kuondoka lakini Mose Iyobo Yupo. Ni Mondi anayejua umuhimu wa Iyobo.
Kuna pisi kali za Mondi zilikuja na kusepa zikamwacha msela huyu fundi wa madansa. Wema, Wolper, Penny, Jojo, Zari, Missa, Tanasha Dona. Wote walikuja himaya ya Mondi na kusepa, Iyobo yupo.
Tukamsifu Mondi kuwa yupo juu kwa miaka 14. Pia tusisahau kando kuna mtu anayemfanya akimbize jukwaani. Mitindo yote ya uchezaji Usafini, huyu ndiye masta wao. Kumbuka pini ya Number One ya kwanza.