Bohari ya Dawa (MSD), inatarajia kuanza kuleta dawa ya kuacha pombe nchini.

MSD inatarajiwa kushirikia na Hospitali Maalum ya Afya ya Akili (Mirembe) iliyopo Jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa MSD, dawa hizo zinatarajiwa kusambazwa katika hospitali zote hapa nchini.

Meneja MSD Kanda ya Dodoma, Mwanashehe Jumaa amesema hayo katika kikao kazi baina ya Wahariri wa vyombo vya habari na MSD kilichofanyika Jijini Dodoma ambako alibainisha kuwa kwa muda mrefu dawa hizo zilikuwa zikipatikana kwa gharama kubwa kutokana kwa taasisi binafsi.

Mwanashee amesema kwa sasa wapo katika hatua za mwisho za ununuzi wa dawa hizo na kwamba tayari wamwshaingia mkataba Hospitali ya Mirembe.

“Hizi ni dawa ambazo MSD hatujawahi kuagiza lakini kutokana na uhitaji tumeona upo umuhimu wa kufanya hivyo, watu wengi sasa Wana changamoto ya afya ya akili,’ amwsisitiza.

Amesema awali dawa hizo zilikuwa zikiuzwa kwa gharama kubwa kwa watoa huduma hivyo uletaji wa dawa hizo utasaidia kundi kubwa la watanzania ambao wanazihitaji.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *