KAMATI ya Mashindano ya Kombe la Muungano imepindua meza, baada ya kufuata mwamuzi Kenya wa kuamua mchezo wa Fainali kati ya Yanga dhidi ya Simba.

Mpaka jioni ya Aprili 28, 2026, kamati hiyo ilikuwa haijamtangaza mwamuzi wa mchezo huo wa Kariakoo Dabi utakaopigwa Jumatano hii ya Aprili 29, 2026 saa 2:15 usiku kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Usiku huu kamati hiyo ikishirikiana na Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) imemtangaza Dickes Mimisa Nyagrowa kuwa mwamuzi wa kati katika mchezo huo.

Nyagrowa raia wa Kenya, kitaaluma ni injinia wa ujenzi mkazi wa Jiji la Mombasa ambapo ndiye atakayesimamia mchezo huo.

Mimisa atasaidiwa na Ally Mbwana atajayekuwa msaidizi wa kwanza, wakati Yusuf Shombe akiwa msaidi wa pili wote wakiwa wanatoka Zanzibar, Isihaka Mwalile akiwa mwamuzi wa nne mezani kutoka Tanzania Bara, huku Ramadhan Kibo akiwa kamishna wa mchezo.

Nyagrowa amewahi pia kuwa mwamuzi kwenye mashindano mbalimbali Afrika yakiwemo Afcon U17 (2023), Afcon U20 (2024), CHAN (2025) na AFCON (2025).

Wakati huohuo, taarifa hiyo imefanya mabadiliko ambapo mgeni rasmi kwenye mchezo huo wa fainali atakuwa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.

Awali kamati hiyo ilimtangaza Makamu wa Rais, Dk Emmanuel John Nchimbi kuwa angekuwa mgeni rasmi lakini sasa imebadilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *