
Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ahmed Attaf amesema Algiers inaunga mkono umoja na mshikamano wa nchi ya Mali kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni ya silaha yaliyolenga maeneo ya kijeshi, akisisitza kuwa nchi yake inapinga “aina zote za ugaidi.”
Attaf kwa mara nyingine tena amesisitiza kuhusu msimamo wa wazi na imara wa serikali ya Algeria katika kuunga mkono umoja, mshikamano, umoja wa kujitawala Mali, wananchi na taasisi za nchi hiyo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali ameeleza haya kupitia taarifa zilizorushwa na kituo cha habari cha kimataifa cha Algeria kinachoendeshwa na serikali cha Al 24 News.
“Algeria “inapinga kikamilifu aina na dalili zote za ugaidi, ambazo haziwezi kuhalalishwa au kuvumiliwa kwa hali yoyote,” amesema Attaf.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria pia ametaka kuimarishwa umoja na mshikamanowa kitaifa ndani ya Mali akisema kuwa suala hilo ni kizuizi bora cha ugaidi.