
Kikosi cha mwisho cha polisi wa Kenya waliotumwa kukabiliana na magenge ya wahalifu nchini Haiti, wamerejea nchini mwao baada ya kuhitimisha misheni yao licha ya makundi yenye silaha kuendelea kudhibiti sehemu kubwa ya Haiti.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kenya iliongoza kikosi cha kimataifa cha usalama kilichoungwa mkono na Umoja wa Mataifa mwishoni mwa mwaka 2023, kusaidia polisi wa Haiti kukabiliana na magenge ya wahalifu.
Hata hivyo, makundi yenye silaha yanasalia katika udhibiti wa maeneo muhimu na yanaendelea kusababisha vurugu kubwa katika taifa hilo la Karibea.
Magenge hayo yamekuwa yakitekeleza mauaji, ubakaji, uporaji na utekaji nyara.
Mwaka jana, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura ya kuubadilisha ujumbe huo kuwa Kikosi chenye nguvu zaidi cha Kukandamiza Magenge (GSF), chenye hadi polisi na wanajeshi 5,500.
Kikosi cha wanajeshi 400 kutoka Chad tayari kimewasili Port-au-Prince, tayari kukabiliana na magenge hayo.