Nchini colombia, mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu mafuta ya visukuku umemalizika Santa Marta. Kufuatia mkutano usio kuwa wa kawada Jumatano alasiri, Aprili 29, nchi 56 zilizoalikwa na Colombia zilitangaza mambo kadhaa muhimu: kuundwa kwa jopo la wanasayansi waliojitolea kupunguza matumizi ya mafuta ya visukuku,  kila nchi kupanga mpito wake wa nishati, na uchambuzi wa vikwazo vya kifedha, ikiwa ni pamoja na deni na ruzuku za mafuta ya visukuku. 

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Santa Marta, Najet Benrabaa

“Wadau wenzangu, wakati ujao tutakuwa hatuuna tena mafuta ya visukuku, si katika nishati wala siasa.” Kwa maneno haya, Waziri wa Mazingira wa Colombia Irene Vélez Torres alihitimisha mkutano wa Santa Marta kwa makofi. Maneno yaliyomvutia Andrea Cardoso, profesa katika Chuo Kikuu cha Magdalena na mtaalamu katika tasnia ya makaa ya mawe. Yeye ni sehemu ya jopo la kisayansi lililoundwa kwa ajili ya tukio hilo.

“Ni mwanzo mzuri, wenye nguvu chanya sana na nia nzuri sana ya kushirikiana kati ya nchi na kati ya wajumbe tofauti. Lengo halikuwa kujadili chochote, tofauti na Mkutano kuhusu tabianchi. Tunataka kuendelea kufanya kazi kwenye mada hiyo. Sote tumefurahishwa na kauli hiyo.”

Kubadilisha nia kuwa vitendo

Changamoto sasa ni kubadilisha nia hii kuwa vite,do. Na hivyo ndivyo hasa Alexandre Naulot, mkuu wa utetezi wa Ulaya kwa Mkataba wa Kutosambaza Mafuta ya Visukuku, anavyotarajia. “Mkutano ujao utaandaliwa na Tuvalu, mwenyeji mwenza wa Ireland. Na zaidi ya yote, Tuvalu ni mwanachama wa majadiliano ya mkataba.” Inatarajiwa kwamba Tuvalu, pamoja na nchi zingine 17 zinazoshiriki katika mazungumzo ya mkataba, wataweka swali la mkataba mpya kwenye ajenda ya mkutano huu.

Washiriki 1,500, mijadala ya siku 5, matukio ishirini yanayofanana. Santa Marta ilitimiza matarajio. Maneno hayo yamesemwa. Sasa yanahitaji kuwekwa katika vitendo—ifikapo mwaka 2027 na kwenda mbali zaidi. Kwa mjumbe wa Ufaransa wa masuala ya hali ya hewa na nishati, Benoît Faraco,anasema matokeo ya mkutano huu ni chanya. “Nilihisi shauku kubwa hapa katika mazungumzo ya hali ya hewa ambayo wakati mwingine huwa magumu na yenye mvutano—kwa sababu sote hatukubaliani. Na hapa, tuna watu wanaotaka kufanya kazi pamoja. Na hilo pia huleta matumaini katika mazungumzo ya hali ya hewa,” anabainisha.

Mjumbe wa Ufaransa wa masuala ya hali ya hewa na nishati anataka kuona mambo katika mtazamo chanya. “Wanasayansi waliokuwepo walitukumbusha kwamba tulikuwa karibu kukosa malengo ya Mkataba wa Paris. Tunaweza kuwa na huzuni kidogo, lakini Mkataba wa Paris ni wa tangu miaka 10 iliyopita… Miaka kumi iliyopita, chanzo cha nishati cha bei nafuu zaidi kwa maendeleo ya kiuchumi kilikuwa makaa ya mawe. Leo, ni nishati ya jua. Hilo ni jambo zuri. Kwa kweli, kuwekeza katika nishati mbadala sasa kutaturuhusu kuokoa pesa baadaye.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *