Mashirika ya haki za binadamu yanalaani mara kwa mara jinsi wafungwa wa Kipalestina wanavyotendewa. Shirika la Physicians for Human Rights–Israel linalaani ukiukwaji mwingine wa haki za msingi. Familia za wafungwa zinakabiliwa na vikwazo vipya katika kufadhili mahitaji ya msingi ya wapendwa wao wanaozuiliwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo lisilo la kiserikali linakadiria kwamba mamia kadhaa ya wafungwa kwa sasa wanaishi bila kupata vifaa muhimu vya matibabu, na maisha ya kila siku yanazidi kuwa magumu kwa baadhi.

Adam Oweineh ana umri wa miaka 24. Kijana huyo ni kiziwi. Akiwa kizuizini bila ya kufunguliwa kesi tangu mwezi Januari 2025, ana kifaa cha kusaidia kusikia, lakini kinahitaji betri ili kufanya kazi. “Kwa zaidi ya mwaka mmoja, amekuwa kizuizini bila kuweza kuwasiliana na mtu yeyote aliye karibu naye. Mamlaka ya magereza haimpi betri.” “Siku moja, mlinzi alipomwita, hakumsikia. Lakini kwa kuwa hakujibu, alipigwa,” anasema Naji Abbas, mkurugenzi wa idara ya wafungwa na mahabusu katika shirika la Physicians for Human Rights–Israel.

Wafungwa wengine wanahitaji miwani, viti vya magurudumu, au magongo. Hapo awali, mamlaka ya magereza lifungua akaunti kwa kila mfungwa, na familia zingeweza kuweka pesa kwa ajili ya vitu hivi, na pia kwa mahitaji mengine ya msingi.

Haki za wafungwa wa Palestina zimevunjwa

“Chakula kinachotolewa na mamlaka ya magereza ya Israel kwa wafungwa wa Palestina hakitoshi.” “Na katika visa kadhaa, Mahakama Kuu imeamua kwamba akaunti hii ya benki, vifaa vidogovidogo kutoka dukani, ni muhimu kwa wafungwa kufurahia kikamilifu haki zao za msingi,” anaongeza Naji Abbas.

Tangu Oktoba 7, 2023, Waziri wa Usalama wa Umma amefunga akaunti hizi kwa wafungwa wa Palestina pekee. Ili kupata pesa, Adam Oweineh sasa anapaswa kumtegemea wakili wake: mchakato mrefu zaidi na wa gharama kubwa zaidi.

Licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwezi Oktoba 2025, miaka miwili baada ya kuanza kwa vita vilivyosababishwa na shambulio la Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7, 2023, Ukanda wa Gaza bado unakabiliwa na vurugu za kila siku. Angalau Wapalestina 800 wameuawa tangu makubaliano hayo yaanze kutekelezwa, kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza, ambayo takwimu zake zinachukuliwa kuwa za kuaminika na Umoja wa Mataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *