Kuelekea uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mwezi Juni mwaka huu, wasimamizi wa uchaguzi waliopatiwa mafunzo ya siku tatu Mkoani Morogoro wametakiwa kutambua uzito wa jukumu lililo mbele yao na kuhakikisha wanayatumia ipasavyo mafunzo hayo ili kusimamia uchaguzi kwa uhuru na haki.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mbarouk Mbarouk, amewasisitiza wasimamizi hao kujikita katika kuisoma na kuielewa Katiba pamoja na sheria za uchaguzi, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi, haki na uadilifu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa mafunzo hayo ambaye pia ni msimamizi wa Jimbo la Nzega Mjini, Omary Mungi, ameahidi kuwa watayafanyia kazi mafunzo yote waliyoyapata ili kuhakikisha uchaguzi huo mdogo unafanyika kwa kuzingatia misingi ya uhuru, haki na uwazi.
(Feed generated with FetchRSS)