Mkuu wa chuo cha Polisi wanamaji Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ndagile Makubi amewataka wananchi waishio kando kando ya ziwa victoria kutoa taarifa za vitendo vya uharifu na waharifu ikiwemo uvuvi haramu ili kulinda rasilimali za taifa.

Makubi amesema hayo katika kijiji cha kigogo wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza wakati wa kutoa elimu ya usalama majini ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya familia ya Polisi

Maadhimisho hayo yameenda sambamba kwa wakufunzi kutoka chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza wametoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili Pamoja na mbinu za kujiokoa Majini.

Awali Makubi katika kuadhimisha siku ya familia ya polisi amewaogoza wakufunzi wa chuo hicho kutoa Msaada wa vyakula na vitu mbali mbali katika makazi ya wazee wasiojiweza yaliyoko Bukumbi.

Askari wa Chuo cha Polisi wanamaji Mwanza wamehitimisha Maadhimisho hayo kwa uongozi chuo kuwatunuku askari sita vyeti vya sifa na zawadi Pamoja na kushiriki michezo mbali mbali.

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *