Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yamewezesha kufanyika kwa mauzo ya papo kwa papo yenye thamani ya shilingi bilioni 3.9 huku zaidi ya asilimia 61 ya waoneshaji wakipata fursa za mauzo ya bidhaa nje ya nchi.

Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Dk. Latifa Mohamed Khamis, amesema hayo wakati wa kufungwa kwa maonesho hayo leo Julai 13, 2026 na kuongeza kuwa, mafanikio hayo yanaonyesha mchango wa maonesho hayo katika kukuza biashara, uwekezaji na kufungua masoko ya kimataifa kwa bidhaa za Tanzania.

Amesema zaidi ya nusu ya bidhaa zilizooneshwa katika maonesho hayo zilizalishwa nchini, hatua inayodhihirisha kuongezeka kwa uwezo wa uzalishaji wa ndani na ushindani wa bidhaa za Tanzania.

Kwa mujibu wa TANTRADE, zaidi ya wananchi elfu 97 walipata huduma mbalimbali za serikali na sekta binafsi kupitia vituo vya huduma vilivyokuwa ndani ya maonesho hayo.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *