#HABARI: Mwenyekiti wa Mama Asemewe, Geofrey Kiliba, amewataka vijana nchini kuwa mstari wa mbele katika kujenga na kulinda agenda ya amani, umoja na mshikamano wa taifa.

Kiliba amesema hayo leo Mei 2, 2026 akizungumza na wanahabari, Kiliba ameeleza kuwa vijana wanapaswa kutumia maarifa waliyonayo kuhubiri amani na kuzuia viashiria vyovyote vinavyoweza kuhatarisha utulivu wa nchi.

“Tuna kila sababu ya kuhakikisha kwa maarifa tuliyokuwa nayo tunajenga agenda ya kuhubiri amani, umoja na mshikamano ndani ya nchi yetu… Taifa hili litakapokuja kuharibika kwa sababu ya kukaa kwetu kimya, watakaoathirika ni sisi wenyewe vijana,” amesema Kiliba.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa vijana kuwa wakweli na wawazi katika kupinga ajenda zozote zisizo na tija kwa taifa, hasa zile zinazoweza kudhoofisha heshima na mshikamano wa Watanzania.
“Ni lazima tuwe wakweli na wawazi kuwaambia kila anayebeba ajenda ya uanaharakati katika misingi isiyo mema… hayo mambo hayakubaliki ndani ya nchi yetu,” ameongeza.

Kiliba ameeleza kuwa vijana wana wajibu wa kuwa kikosi cha mbele katika kulinda tunu za taifa, akiwataka wasikubali kutishwa, kunyamazishwa au kupotoshwa pale wanapoona viashiria vya kuhatarisha amani.
“Asitokee mtu yoyote akakunyamazisha na kukukosesha nguvu za kukemea mahala ambapo unaona kuna viashiria vya kuondosha amani,” amesisitiza.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *