#HABARI: Tanzania imeandika historia mpya katika sekta ya nishati safi baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa na wa kwanza Afrika Mashariki wa kuzalisha nishati ya umeme kwa nishati ya jua ulioko Kishapu Mkoani Shinyanga, ikiwa ni ushahidi wa dhamira thabiti ya Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme wa uhakika kwa Watanzania.

Jumla ya shilingi Bilioni 118.6 zimetajwa kutumika katika mradi huo kwa awamu ya kwanza, ukizalisha Megawati 50 ambazo zimeunganishwa kwenye gridi ya Taifa, awamu ya pili ikielezwa kuanza hivi karibunk kwa kuzalisha Megawati 100 ambazo zitagharimi takribani Shilingi Bilioni 204 na hii ni kulingana na Meneja wa mradi huo kutoka Tanesco Mhandisi Emmanuel Anderson.

Wananchi wa Kishapu wamemshukuru Rais Samia kwa utekelezaji wa mradi huo katika eneo lao, wakieleza kuwa mbali na ajira nyingi kutoka kwa Vijana wa eneo hilo, fidia zilizotolewa kwa wananchi waliopisha mradi huo zimesaidia kuinua uchumi wa wananchi wengi na kuendeleza Mji huo kwa kiasi kikubwa kwani umechochea kasi ya maendeleo ya Viwanda na shughuli za kiuchumi.

Kulingana na wasimamizi wa mradi huo, umeme unaozalishwa hapo utaongeza uwezo wa uzalishaji kwenye gridi ya Taifa na kuboresha ufanisi wa huduma kwa wateja, mradi ukitajwa kama alama ya mabadiliko makubwa na hatua muhimu katika muelekeo wa Tanzania kutumia matumizi ya nishsti jadidifu katika uzalishaji wa umeme, hatua inayolenga kuimarisha usalama wa nishati.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *