MRATIBU wa Simba Queens, Selemani Makanya ameweka wazi mafanikio ya timu hiyo kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake yanatokana na mipango waliyojiwekea tangu mwanzo wa msimu.

Simba Queens iliyo kileleni mwa msimamo wa ligi na pointi 43, kwenye mechi 15 imeshinda 14 na sare moja, ikiwa haijapoteza mechi hata moja rekodi inayoiweka kwenye nafasi nzuri ya kurejesha ubingwa unaotetewa na JKT Queens.

Makanya amesema msimu huu ni mgumu kutokana na kila timu kuwa na hamasa ya kuifunga Simba Queens, jambo linalowalazimu kuwa makini zaidi katika kila mechi.

MAKA 01 (1)

“Ni msimu mgumu sana kwa sababu kila timu inapambana kufanya vizuri dhidi yetu. Ukiteleza tu kwenye mechi moja, hali inakuwa ngumu zaidi,” amesema Makanya.

Ameongeza siri nyingine ya mafanikio ni kufanya usajili mkubwa wenye kuzingatia mahitaji halisi ya kikosi, hasa pale mchezaji anaposhuka kiwango.

“Mchezaji anapopungua kiwango, lazima uwe na mbadala sahihi wa kuziba pengo lake, ndiyo maana tulifanya usajili mkubwa msimu huu ukilenga mahitaji ya timu.”

“Tuna malengo makubwa. Kwanza ni kurudisha ubingwa wetu, pia tunataka kurejea kwenye michuano ya kimataifa. Kikosi chetu kina uwezo wa kufanya makubwa,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *