LICHA  ya Simba Queens kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu wa 2025/26, kuna presha ya kuwania ubingwa kwa Yanga Princess na JKT Queens zinazoendelea kukimbiza kimya kimya.

Kwa mujibu wa msimamo wa ligi hadi raundi ya 15, Simba Queens inaongoza kwa pointi 43 ikiwa haijapoteza mchezo wowote, huku Yanga Princess ikiwa nafasi ya pili na pointi 39.

Tofauti ya pointi nne imezifanya mbio za ubingwa kuchukua sura mpya, huku Yanga ikiwa na safu kali ya ushambuliaji iliyotikisa nyavu mara 44 ikiwa ndiyo timu pekee iliyofunga mabao mengi na Simba ikiwa na beki imara iliyoruhusu mabao mawili hadi sasa.

VIT 01

Nafasi ya tatu inashikiliwa na JKT Queens yenye pointi 38, ikiwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Yanga, hali inayozidi kuchochea ushindani katika nafasi za juu.

Chini ya msimamo, hali si shwari kwa Bilo FC inaoshika mkia kwa pointi tano na Ruangwa ikiwa nafasi ya 11 na pointi nane, inahitaji kupambana zaidi ili kujinusuru kushuka daraja.

VIT 02

Ikumbukwe timu hizo zilipanda daraja msimu huu baada ya kufanya vizuri Ligi Daraja la kwanza na sasa zinapambana kujinasua kushuka daraja.

Ili zisalie kwenye ligi zinahitaji kushinda mechi zote saba zilizosalia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *