Nchini Morocco, wanajeshi wawili wa Marekani hawajulikani waliko baada ya kukosekana karibu na mji wa kusini wa Tan-Tan siku ya Jumapili, Mei 3. Walikuwa wakishiriki katika mazoezi ya pamoja ya African Lion 2026. Vikosi vya jeshi wiliwakosa Jumamosi usiku. Washington inahofia kwamba huenda walidondoka katika Bahari ya Atlantiki.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mazingira ya tukio hilo bado yanachunguzwa, kulingana na vikosi vya Kifalme vya Morocco pamoja na Africom, Kamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika.

Operesheni imezinduliwa ili kuwapata wanajeshi wawili wa Marekani waliotoweka Jumamosi usiku, Mei 2, anaripoti mwandishi wetu huko Casablanca, François Hume-Ferkatadji. Shughuli za utafutaji wa kina zimeanzishwa, zikihamasisha jeshi la ardhini, anga, na baharini vya Marekani na Morocco, pamoja na wanajeshi kutoka nchi kadhaa washirika. Tan-Tan, jiji lililoko kusini mwa Morocco, linapatikana takriban kilomita 25 kutoka Bahari ya Atlantiki.

Jeshi la Marekani linashuku ajali. “Ninaweza kuthibitisha kwamba tukio hili halihusiani na ugaidi lakini linaonekana kuwa ajali,” afisa wa jeshi la Marekani ameliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina. Kulingana na chanzo hiki na matokeo ya awali, “wanajeshi hao wawili huenda walidondoka baharini.” Kulingana na jeshi la Morocco, wanajeshi wa Marekani walitoweka karibu na mwamba, karibu na eneo la mafunzo la Cap Draa.

Mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka, yanayojulikana kama African Lion, ni mazoezi makubwa zaidi ya pamoja kati ya Kamandi ya Marekani barani Afrika, washirika wake wa NATO, na washirika wake wa Afrika. Yanafanywa ili kuimarisha ushirikiano kati ya majeshi mbalimbali husika.

African Lion sasa iko katika mwaka wake wa 22. Toleo la 2026 litafanyika kuanzia Aprili 27 hadi Mei 8 katika nchi nne: Ghana, Morocco, Senegal, na Tunisia. ILinajumuisha takriban wanajeshi 5,000 kutoka zaidi ya nchi 40.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *