
Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wakati nchi hiyo ilikuwa ikisubiri kutangazwa kwa matokeo ya muda ya duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge wa Aprili 26, 2026, Jumatatu, Mei 3, matokeo, hatimaye, hayakutangazwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Bangui, Rolf Steve Domia-leu
Kulingana na kanuni za uchaguzi, matokeo haya yanaweza kuwekwa hadharani ndani ya siku nane baada ya uchaguzi. Vikiwasiliana na RFI, baadhi ya vyanzo vya ndani vimebainisha kwamba matokeo hayo yamezuiwa ndani ya Mamlaka ya Kitaifa ya Uchaguzi (ANE). Wafanyakazi wa IT katika kituo cha usindikaji data cha chombo hiki wanaripotiwa kuzuia matokeo. Wanadai malipo ya mishahara ya miezi miwili ya nyuma. Kwa hivyo nchi inabaki katika mashaka ikisubiri matokeo haya, ambayo sasa yameahirishwa hadi itakapotangazwa tarehe ningine.
Mamlaka ya Uchaguzi (ANE) inabainisha kwamba shughuli zake zote kwa sasa zimesimama. Inatangaza ufunguzi wa majadiliano na wafanyakazi waliogoma ili kupata suluhisho la haraka. Mnamo mwezi Aprili 2026, wafanyakazi walidai malipo ya mishahara ya miezi miwili ya nyuma kabla ya duru ya pili ya uchaguzi. Makubaliano yalifikiwa kati ya pande hizo mbili.
“Mchezo mchafu”
“Ahadi zilizovunjwa, ambazo zinafanana kama mchezo mchafu,” mtaalamu wa IT katika kituo cha usindikaji data cha ANE amekiri kwa sharti la kutotajwa jina. Siku nane baada ya uchaguzi wa Aprili 26, wafanyakazi waliamua kuongeza shinikizo. “Tuliamua kuzuia matokeo. Tunadai malipo ya mishahara yetu kabla ya kutangazwa,” mfanyakazi huyu ameongeza.
Kuingilia Kati na kupata suluhisho
Waangalizi wengi na wadau wa mashirika ya kiraia wanatoa wito kwa mamlaka na washirika kuingilia kati kwa ajili ya suluhisho la haraka la mgogoro huo. Licha ya matokeo ambayo hayajachapishwa ya duru ya pili, wabunge waliochaguliwa katika duru ya kwanza walianza rasmi vikao vyao Jumatatu, Mei 3. Kikao hiki kisicho kuwa cha kawaida, ambacho kinatarajiwa kudumu hadi Mei 18, kimetengwa kwa ajili ya kuwekwa kwa wabunge, kuanzishwa kwa ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), pamoja na kuundwa kwa kamati za kudumu na makundi ya wabunge.