Sudan imemrejesha nyumbani balozi wake nchini Ethiopia kwa mashauriano, ikiituhumu nchi hiyo kuhusika katika shambulio la uwanja wa ndege wa Khartoum pamoja na Falme za Kiarabu, shirika la habari la serikali, SUNA limeripoti leo Jumanne.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wimbi la mashambulizi ya ndege zisizo na rubani lililenga uwanja wa ndege wa Khartoum na maeneo mengine kadhaa ya kimkakati mnamo Mei 4, 2026. Hii ni mara ya pili katika siku kumi ambapo wanamgambo wa Sudan kutoka Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) wamelenga mji mkuu, ambao uko chini ya udhibiti wa jeshi la serikali.

Kulingana na mamlaka ya Sudan, mashambulizi hayo hayakusababisha majeruhi, lakini uwanja wa ndege ulifungwa kwa saa 72 na wafanyakazi na abiria waliondolewa katika majengo ya serikali kwa hofu ya mashambulizi zaidi.

Kulingana na jeshi la Sudan, makombora manne yalilenga uwanja wa ndege. Mawili yalidondoka kwenye jengo la utawala lililoko mashariki mwa eneo la bandari. Ndege zingine mbili zisizo na rubani zilishambulia nyumba zilizo karibu. Mashahidi walirekodi na kushiriki kwenye safu za mitandao ya kijamii za moshi mweusi ukipanda angani. Kulingana na jeshi, maeneo mengine, kama vile kambi ya kijeshi ya Omdurman na kambi ya Khartoum-Bahri, pia yalilengwa. Baadhi ya ndege zisizo na rubani zilidondoshwa. Hakuna hasara kwa upande wa raia ilyioripotiwa.

Khartoum imerejesha shutuma zake dhidi ya Ethiopia, ambayo inashuku kuunga mkono wanamgambo wa Sudan wanaodai kwamba ndege hizi zisizo na rubani za masafa marefu zilirushwa kutoka kambi ndani ya eneo la Ethiopia.

Ndege zisizo na rubani zimeshambulia maeneo mengine ya nchi

Tangu wiki iliyopita, ndege zisizo na rubani za RSF zimeshambulia maeneo kadhaa huko North Kordofan, Blue Nile, Gedaref mashariki mwa Sudan, na al-Jazira katikati mwa Sudan. Katika jimbo hili, ambako inaishi familia ya Kamanda Abu Akla Kikel, mshirika wa jeshi na mkuu wa kikosi cha “al-Jazira Shield”, ililengwa siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita. Watu tisa waliuawa, wakiwemo ndugu zake wawili na kamanda mmoja kutoka jeshi lake.

Nyumba hiyo iko kama kilomita 40 mashariki mwa Wad Madani, mji mkuu wa al-Jazira.

Abu Akla Kikel alikuwa kamanda wa zamani wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika Jimbo la al-Jazira kabla ya kuhama. Alijiunga tena na jeshi mnamo mwezi Oktoba 2024 na kikosi kizima alichokiongoza. Anashutumiwa kwa ukatili kutoka pande zote mbili katika mzozo huo.

Jeshi la Sudan na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) ambao wanapigana tangu mwezi Aprili 2023,  wameongeza mashambulizi yao ya ndege zisizo na rubani katika miezi ya hivi karibuni, wakati mwingine wakiua makumi ya watu. Siku ya Jumamosi, shambulio la wanamgambo liliwaua watu watano katika mji mkuu wa Sudan.

Mnamo mwezi Machi, serikali ya Sudan inayounga mkono jeshi iliripoti mashambulizi ya ndege zisizo na rubani “yaliyoendeshwa kutoa katika ardhi ya Ethiopia,” shutuma isiyo ya kawaida dhidi ya nchi jirani. Addis Ababa ilikana madai hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *