#HABARI: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, ameilekeza TARURA na Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha ujenzi wa barabara ya Togo unakamilika ifikapo Juni 2026.
Prof. Shemdoe ametoa maelekezo hayo leo Mei 10, 2026, jijini Dar es Salaam, huku akiagiza mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kimario (Brazil) usainiwe ifikapo Mei 25, ili kuanza kutatua kero za usafiri kwa wananchi wa maeneo hayo.
Waziri amewataka mameneja wa TARURA mkoa na wilaya kusimamia miradi hiyo kwa ukaribu ili ikamilike kwa kiwango cha lami kupitia mradi wa DMDP II, hususan katika kipindi hiki cha mvua.
Amesema serikali haitakubali ucheleweshaji wowote na amewasisitiza madiwani kufuatilia utekelezaji wa maagizo hayo ili kuhakikisha watumiaji wa barabara hizo wanapata nafuu ya usafiri haraka iwezekanavyo.
Aidha, Prof. Shemdoe amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kugharamia ujenzi wa barabara 17 wilayani Kinondoni zenye urefu wa kilometa 36 zilizogharimu shilingi bilioni 97.7.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Abbas Tarimba, amempongeza Waziri kwa usikivu wake na kujitolea kufanya ziara hiyo siku ya Jumapili ili kusikiliza kero za wananchi na kutoa ufumbuzi wa kudumu wa miundombinu jimboni humo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)