Dar es Salaam. Una ‘stresi’? Za mapenzi, ugumu wa maisha ama chochote. Fanya hivi, kama huna akaunti ya Insta basi fungua leo. Na kama unayo basi ‘mfolo’ Stan Bakora. Utarudi hapa tena kunishukuru kwa hili la kukusanua.

Mara ya kwanza naigumia ‘posti’ yake, nilicheka lakini sikudhani kama itakuwa hivi ilivyo. Mchizi amekuja na ubunifu flan hivi wa kindezi sana. Usipocheka ndugu utakuwa na matatizo mazito ya afya ya ubongo.

Naona baadhi wanaiga ubunifu wake lakini hawana karama. Ni Stan Bakora na mwanaye mmoja hivi. Wamekuja na kitu cha pekee kinachoumiza mbavu za wengi. Anachekesha kiasi kwamba hata yeye anacheka akichekesha.

Vichekesho vyake ni vifupi sana. Lakini vinakuacha na kicheko cha muda mrefu sana. Ogopa mtu anayekuchekesha sana kiasi cha kukulazimisha ‘ukomenti’ katika ‘posti’ husika. Hata kwa ‘imoji’ tu, ni vichekesho shawishi.

Stan Bakora yupo katika dunia ya peke yake kwa sasa. ‘Komenti’ na ‘laiki’ za waja, zitakupa uhalisi wa kuiteka jamii yake kwa jambo lile analofanya. Sishangai wanaoiga kuwa ni ubunifu wa kipekee sana ambao unatamani uanze wewe.

Kwa akili ya namna hii, huwezi kulala njaa kwenye uso wa dunia ya sasa. Ni vitu vinavyoenda na wakati huu wa dunia ya ‘mastresi’ mengi na mingiliano wa mambo kichwani. Stan Bakora deile Insta anakua sababu ya kufurahi.

Stan Bakora ndo ‘stresi rimuva’ kwa sasa. Hii dunia inawahitaji watu sampuli ya Stan Bakora ili kupunguza matatizo mengi ya afya ya akili. Watu wengi hudedi kwa ubwege wa kuwaza ujinga wa shida za kijinga. Cheka!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *