Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amelitaka Jeshi la Polisi Nchini kuimalisha doria za mitandaoni ili kuwabaini waharifu wanaotumia mitandao kuibia wananchi.

Mtanda ametoa maelekezo hayo kwenye maadhimisho ya siku ya familia ya polisi iliyofanyika katika viwanja vya nyamagana jijini Mwanza.
Aidha mtanda katika hotuba yake akatoa maagizo kwa askari na maafisa wa Polisi.

Akielezea Umuhimu wa siku ya familia ya Polisi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi Wilbroad William Mtafungwa amesema Jeshi la Polisi litaendelea kufanya kazi zake kwa Weledi.

Maadhimisho hayo yalianza kwa Mtanda kukagua Gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake

baada ya gwaride Mtanda alikagua maonyesha ya kazi za Polisi ikiwemo usalama barabarani ,Polisi wananamaji pamoja na Kitengo cha Mbwa.

Siku ya familia ya Polisi imehitimishwa kwa michezo mbali mbali iliyofanyika katika viwanja wa Nyamagana.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *