Serikali imeanza mkakati wa kuimarisha usuluhishi wa migogoro ya ndoa ngazi ya jamii, hatua inayolenga kupunguza talaka na kupunguza mzigo wa mashauri mahakamani.
Kupitia mafunzo yaliyotolewa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, wajumbe wa bodi za usuluhishi wa ndoa wamejengewa uwezo wa kushughulikia migogoro kwa weledi, kwa lengo la kurejesha amani ndani ya familia kabla migogoro haijafika mahakamani.
Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, James John amesema suluhisho la kudumu la migogoro ya ndoa linaanzia kwenye jamii, akisisitiza kuwa wajumbe hao wanapaswa kutoa ushauri unaolenga kuzuia migogoro badala ya kusubiri kuisuluhisha baada ya kuharibika.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Musa Gumbo amesema mafunzo hayo ni hatua muhimu ya kujenga mifumo madhubuti ya usuluhishi itakayosaidia familia nyingi kubaki imara na kupunguza migogoro isiyo ya lazima.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)