Ukisikia Hakuna marefu yasiyo na ncha Tafsiri yake utaipata mitaa ya Twiga na Jangwani nyumbani kwa mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, baada ya kucheza michezo 40+ pasina kupoteza mchezo wowote, leo imekuwa tofauti mbele ya walima Zabibu wa Dodoma timu ya Dodoma Jiji baada ya kukubali kipigo cha magoli matatu huku wananchi wakiambulia mawili. (3 – 2)

Kipigo hiki kinafufua matumaini ya mnyama Simba Sc kuelekea mbio za ubingwa amabapo siku ya alhamisi 14 may 2026 Simba itakuwa Ugenini Mkoani Kigoma kukipiga dhidi ya Mashujaa ya mkoani humo katika Dimba la Lake Tanganyika.

Unalia/Unacheka ukiwa mkoa Gani?

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *