
Wakati AFC/M23 inayoungwa mkono na Rwanda ikiondoka wiki hii kutoka maeneo kadhaa katika Uwanda wa Ruzizi na nyanda za juu za mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa DRC, shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) linalishutumu kundi hilo lenye silaha na vikosi vya Rwanda kwa ukatili wakati wa kukamatwa na kukaliwa kwa mji wa Uvira mnamo mwezi Desemba 2025.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
M23 nawanajeshi wa vikosi vya Rwanda waliingia Uvira (DRC) mnamo Desemba 10, 2025, baada ya siku kadhaa za mapigano dhidi ya jeshi la Kongo—na wanamgambo washirika wa Wazalendo—na kuuteka mji huo kwa mwezi mmoja. Kulingana na HRW, wapiganaji wao walifanya ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu, ambazo nyingi ni uhalifu wa kivita.
Kulingana na ushuhuda uliokusanywa na HRW, wapiganaji hawa waliwapiga risasi raia waliojaribu kukimbia, wakiwemo wanaume na wavulana wanaotuhumiwa kuwa wanamgambo wa Wazalendo. Shahidi mmoja anasimulia jinsi kaka yake, mkewe, na watoto wao wawili walivyouawa kwa kupigwa risasi katika kitongoji cha Kavimvira walipokuwa wakijaribu kukimnilia nchi jirani ya Burundi.
Mauaji ya kikatili na ubakaji
Shahidi mwingine anaelezea jinsi wapiganaji hawa walivyowapiga risasi wavuvi katika bandari ya kitongoji cha Kasenga kutoka kwenye paa za majengo. Ripoti ya HRW pia inarekodi mauaji ya kikatili na ubakaji wakati vikosi vya M23 na Rwanda vikienda nyumba kwa nyumba, haswa katika vitongoji vya Kasenga na Rugenge.
Hatimaye, shirika hilo linaripoti kutekwa nyara na kutoweka kwa wanaume na wavulana karibu na kituo cha kijeshi cha Uvira ambao huenda waliajiriwa kwa nguvu na M23.