Maambukizi mapya ya virusi hatari vya Ebola, yamethibitishwa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika (CDC Africa).

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Watu 246 wanahofiwa kuambukizwa huku wengine 65 wakithibitishwa kufariki dunia baada ya mlipuko wa ugonjwa huo, katika mkoa wa Ituri.

Watu wanne waliopoteza maisha na kufanyiwa vipimo kwenye maabara wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola.

“Tunathibitisha mlipuko wa virusi vya Ebola mkoani Ituri” kituo cha CDC Afrika kimesema katika taarifa yake.

Kituo hicho kimesema kinafuatilia mwenendo wa maambukizi hayo, na kutoa wito kwa mataifa jirani za Uganda na Sudan Kusini, kuimarisha uangalizi mipakani kuzuia ugonjwa huo kusambaa.

Hii sio mara ya kwanza kwa virusi vya Ebola kuripotiwa nchini DRC, kati ya mwaka 2018 na 2020 ugonjwa huo ulisababisha vifo vya watu karibu 2,300.

Ugonjwa huu unaosambaa kwa haraka kati ya binadamu, umewauwa watu 15,000 katika mataifa mbalimbali barani Afrika katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *