KOCHA wa makipa wa timu ya Polisi, Ali Masoud, amesema kikosi hicho kipo tayari kwa michezo iliyosalia Ligi Kuu Zanzibar ili kujinusuru kushuka daraja msimu huu.

Kauli ya kocha huyo imekuja baada ya Kamati ya Mashindano ya Bodi ya Ligi kuipa Polisi ushindi wa point tatu na mabao mawili kufuatia wapinzani wao KMKM katika mchezo nambari 191 kushindwa kufika uwanjani wakiwa na wachezaji wanaostahili kucheza. Katika hilo, KMKM imetozwa faini ya Sh3 milioni.

Kocha huyo amekiri timu hiyo kutokuwa kwenye nafasi nzuri kwani ipo kwenye mstari wa kushuka daraja nafasi ya 13 lakini amesema mipango ya kuinusuru ipo.

POLI 01

“Hatupo kwenye nafasi nzuri, bado tunajiweka sawa na kutafuta njia bora ya kutumia kusalia ligi Kuu,” amesema.

Kocha huyo, amesema kila timu kwa sasa inaangalia namna ya kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi, jambo ambalo linaongeza ushindani mkubwa kwa michezo yote.

Naye Nahodha Msaidizi wa Polisi, Mgeni Silima, amesema malengo yao kwa sasa ni kuhakikisha wanapata pointi tatu katika kila mchezo.

POLI 02

Amesema, ushindi walioupata dhidi ya KMKM umeongeza morali kwa wachezaji na kuwapa ari mpya ya kuendelea kufanya vizuri katika michezo inayofuata.

Polisi imebakiwa na mechi tano kumaliza msimu huu ambapo sasa inashika nafasi ya 13 ikikusanya pointi 29, imebaki eneo la mstari mwekundu wa kushuka daraja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *