Mnunka: Simba Queens tunataka kurudi AfrikaMnunka: Simba Queens tunataka kurudi Afrika

KIUNGO mshambuliaji wa Simba Queens, Aisha Mnunka amesema lengo kubwa la timu hiyo msimu huu ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania na kurejea katika michuano ya kimataifa baada ya kukosa nafasi hiyo mwaka uliopita.

Simba imeendelea kuonyesha ubabe kwenye ligi msimu huu baada ya kucheza mechi 16 bila kupoteza hata moja, ikishinda 15 na kutoka sare moja. Matokeo hayo yameifanya kuongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 46, ikizipita wapinzani wake wa karibu, Yanga Princess na JKT Queens, kwa tofauti ya pointi saba.

Mnunka, ambaye hadi sasa amefunga mabao manane, amesema kila mchezaji ndani ya kikosi hicho anatambua umuhimu wa mechi zilizobaki na wanahitaji kuendelea kupambana hadi dakika ya mwisho ili kuhakikisha wanarudisha taji Msimbazi.

MNUNK 01

“Ndoto yetu kubwa ni kurudi kucheza michuano ya kimataifa. Ili tufanikishe hilo, lazima tushinde ubingwa wa ligi. Tunajua kazi bado haijaisha kwa sababu zimesalia mechi muhimu ambazo zitatoa picha halisi ya bingwa wa msimu huu,” amesema Mnunka.

Kiungo huyo ameongeza morali ya wachezaji ipo juu kutokana na mwenendo mzuri wa timu, huku kila mmoja akiwa tayari kutoa mchango wake kuhakikisha Simba inamaliza msimu ikiwa juu ya msimamo.

Katika mechi sita zilizobaki, Simba itavaana na Ruangwa Queens kabla ya kukutana na JKT katika mechi inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Baadaye itacheza dhidi ya Tausi FC, Mashujaa Queens, Alliance Girls na kumalizia msimu dhidi ya Geita Queens.

Mchezo dhidi ya JKT unatajwa kuwa mmoja wa mechi muhimu zaidi katika mbio za ubingwa, kwani unaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa nafasi ya Simba kutwaa taji hilo.

MNUNK 02

Kama Simba itachukua ubingwa na kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Cecafa kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake itakuwa mara yao ya tatu kufanya hivyo.

Tangu michuano hiyo ianzishwe mwaka 2021 Simba imecheza mara mbili mwaka 2022 Simba ilinyakua ubingwa kisha kufika hadi nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Mwaka 2023 JKT iliwakilisha Tanzania ikaishia hatua ya makundi na mwaka 2024 Simba ikarejea tena kwenye hatua za kufuzu ikaishia nusu fainali ya Cecafa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *