Darmanin kuzuru Algiers, hatua mpya katika mahusiao kati ya Ufaransa na AlgeriaDarmanin kuzuru Algiers, hatua mpya katika mahusiao kati ya Ufaransa na Algeria

Gérald Darmanin atasafiri kwenda Algiers Jumatatu kwa ziara fupi inayolenga “kurejesha uhusiano wa kimahakama” kati ya Ufaransa na Algeria.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Akiwa amealikwa na mamlaka ya Algeria, Gérald Darmanin anawasili katika mji wa Algeria, leo Jumatatu, Mei 18, akiambatana na mahakimu kadhaa wakuu wa Ufaransa, kwa lengo moja: kufufua ushirikiano wa kimahakama ambao umesitishwa. Hali ya mwandishi wa habari za michezo Christophe Gleizes, aliyekamatwa nchini Algeria kwa zaidi ya mwaka mmoja, itajadiliwa. Lakini katikati ya mazungumzo hayo kuna kesi nyeti: biashara ya dawa za kulevya na utakatishaji fedha.

Gérald Darmanin anataka majina na taarifa kuhusu wafanyabiashara kadhaa wa dawa za kulevya wanaoshukiwa kuwa wamekimbilia Algeria au kuwa na fedha zilizofichwa huko. Hasa, anawalenga takriban watu kumi muhimu katika DZ Mafia, shirika la jinai lenye vurugu kubwa  linalosababisha umwagaji damu huko Marseille na kugonga vichwa vya habari nchini Ufaransa kwa kulipiza kisasi na kurusha risasi hovyo.

Paris inatarajia kupata kutoka Algiers kile ambacho imefanikiwa kufikia na Falme za Kiarabu na Morocco: wahaliu kukamatwa, kunyang’anywa mali zao, na hatimaye kuhamishiwa nchini Ufaransa. Ushirikiano huu ulianzishwa chini ya uongozi wa Vanessa Perrée, mwendesha mashtaka anayehusika na kupambana na uhalifu uliopangwa, ambaye aliandamana na ujumbe huo hadi Algiers. Pia katika ziara hiyo yuko Pascal Prache, mkuu wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka mkuu wa Fedha. Mahakimu hawa wawili wa ngazi ya juu ni ishara ya kujitolea kwa dhati kwa ushirikiano thabiti.

Kwa karibu miaka miwili, kutokana na mvutano wa kidiplomasia, ubadilishanaji wa taarifa ulisitishwa. Wale walio karibu na Waziri wa Sheria wanakosoa waziwazi mkakati wa makabiliano uliofuatwa na Bruno Retailleau alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Gérald Darmanin atakuwa na mbinu tofauti ya kuanzisha, kesi kwa kesi, hatua inayowezekana ya mabadiliko katika mahusiano ya Ufaransa na Algeria.

Kwa kubadilishana, Algiers inatarajiwa kuwasilisha madai yake, hasa kuhusu kesi za za utakatishaji fedha. Kwa vyovyote vile, ziara hii ya tatu ya waziri wa Ufaransa nchini Algeria tangu mwanzo wa mwaka inaonekana kuashiria kwamba uhusiano kati ya Paris na Algiers unarudi katika hali yake ya kawaida baada ya karibu miaka miwili ya mgogoro wa kidiplomasia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *