
Zambia ilivunja Bunge lake Ijumaa, Mei 15, chini ya miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa urais mnamo Agosti 13. Kuvunjwa kwa bunge hili kumezua maswali na wasiwasi miongoni mwa mashirika ya kadhaa za kiraia.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kuvunjwa kwa bunge kunakuja baada ya kumalizika kwa kikao cha bunge kilichokumbwa na vurugu kubwa: sheria 73 zilichunguzwa na kupitishwa katika wiki moja tu. Sheria hizi, zinazohusu usalama wa mtandao, mikusanyiko ya umma, na ufuatiliaji, ambazo zinachukuliwa na mashirika kadhaa kuwa zinatia wasiwasi kuhusu uhuru wa raia.
“Hatujui nia za kupitishwa kwa sheria hizi zote katika wiki moja, wakati tulikuwa na miaka mitano ya kufanya kazi hii ipasavyo,” anasema Austin Kayanda, mkurugenzi wa Taasisi ya Media Institute of Southern Africa, aliyehojiwa na Christina Okello. Akizungumza na RFI, mwakilishi huyo wa mashirika ya kiraia anakumbusha kwamba wasiwasi ulikuwa umeibuka kuhusu hitaji la kupitia baadhi ya sheria hizi tangu mwanzo wa muhula, “na tulihakikishiwa kwamba hili halitatokea,” anaelezea.
Kwa nini sasa? Katika muda mfupi kama huo? Austin Kayanda anabaini kwamba Wazambia walipaswa kuwa na muda zaidi wa kupitia maandishi haya na kutoa maoni yao. Sheria moja hasa ndio inaleta tatizo: ile inayohusu mikusanyiko ya umma. “Hii ina maana kwamba tunarudi kwenye enzi ya ukoloni, ambapo idhni ilihitajika ili kukutana, kukusanyika au kushiriki mawazo. Kwetu sisi, sheria hii haina tofauti na sheria kuhusu usalama na utulivu wa umma ambayo ilitakiwa kuchukuxa nafasi yake,” anasema.
Austin Kayanda sasa anatumai kwamba Rais Hakainde Hichilema hatatangaza baadhi ya sheria hizi, “ili raia wawe na muda zaidi wa kuzipitia na kushiriki katika mjadala.”
Hatujui nia za kupitisha sheria hizi zote katika wiki moja, wakati tulikuwa na miaka mitano ya kufanya kazi hii ipasavyo. Tangu mwanzo wa muhula wake, wasiwasi uliibuka kuhusu hitaji la kupitia baadhi ya sheria hizi, na tulihakikishiwa kwamba hili halingetokea. Kisha, ghafla, zilirudishwa mezani na kupelekwa Bungeni. Raia walipaswa kuwa na muda zaidi wa kuchunguza sheria hizi na kutoa maoni yao. Miongoni mwa sheria 73 zilizopitishwa ni muswada wa mikusanyiko ya umma… Hii ina maana kwamba tunarudi kwenye enzi ya ukoloni, ambapo idhni ilihitajika ili kukutana, kukusanyika au kushiriki mawazo. Kwetu sisi, sheria hii haina tofauti na sheria kuhusu usalama na utulivu wa umma ambayo ilitakiwa kuchukuxa nafasi yake.
