Steve Barker akomaa SimbaSteve Barker akomaa Simba

INGAWA Simba ipo nyuma kwa pointi mbili dhidi ya Yanga iliyopo kileleni kwa alama 54, hiyo siyo ishu inayompasua kichwa Kocha mkuu Steve Barker, ambaye hesabu zake ni kuhakikisha ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu unatua mitaa ya Msimbazi.

Barker ndiye kocha aliyebadili upepo wa Simba kufungwa kila ilipokuwa inakutana na Yanga na ameisaidia msimu huu kanyakua taji la Muungano 2026 ikishinda dabi dhidi ya Yanga, huku pia zilipokutana kwenye ligi, Machi Mosi 2026 ilikuwa 0-0 na ya Mei 3, 2026 zilitoshana nguvu kwa mabao 2-2.

Barker alisema jambo la msingi kwake siyo timu kuzidiwa pointi mbili na Yanga, bali ni kuhakikisha wanashinda mechi zilizosalia mbele yao, zitakazobadilisha ndoto za ubingwa na kuwa halisi.

“Kila mechi kwetu ni muhimu tushinde, tunapokutana timu mbili uwanjani tayari ni ushindani wa kutafuta pointi tatu, umakini wetu upo katika kushinda na siyo jambo lingine, kwani ubingwa unawezekana ni kupambana hadi dakika ya mwisho,” alisema kocha huyo na kuongeza;

“Natambua ligi ni ngumu na yenye ushindani kila tunapocheza mechi tunafanya tathimini itakayotupa matokeo chanya ya mbele.”

Simba chini ya Barker aliyetambulishwa Desemba 19, 2026, zimechezwa mechi 20, timu hiyo imeshinda 13 na sare saba, haijapoteza huku ikivuna pointi 46, jambo ambalo anaamini ubingwa bado upo wazi kwa upande wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *