Samia ateua majaji tisa Mahakama ya RufaniSamia ateua majaji tisa Mahakama ya Rufani

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewateua majaji tisa kuwa majaji wa Mahakama ya rufani.

Awali, Mahakama ya Rufani ilikuwa na jumla ya majaji 40 kwa mujibu wa taarifa za Mahakama.

Taarifa ya uteuzi huo, imetolewa leo, Jumatano Mei 20, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka na kutiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, walioteuliwa ni Abdi Kagomba, aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Yohane Masara aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na Immaculata Banzi aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kagera.

Wengine walioteuliwa ni Rabia Mohamed aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Cyprian Mkeha aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara Dar es Salaam na Yose Mlyambina aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Dar es Salaam.

Pia, wamo Imani Aboud aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Mzee Ibrahim aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar na Juliana Masabo aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wateule hao wataapishwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *