
Viongozi wa China na Russia wamesisitiza mwanzoni mwa mazungumzo yao kuhusu azimio la pamoja la nchi hizo mbili la kuasisi utaratibu wa haki zaidi wa kimataifa na ulimwengu wa kambi kadhaa.
Rais Xi Jinping wa China amemtaja Rais Vladimir wa Russia kuwa rafiki wa muda mrefu na kubainisha kuwa: Kwa mianga mingi wawili hao wamedumisha uhusiano wa karibu na kuweka wazi namna ya kuimarisha na kuendelea uhusiano kati ya China na Russia kwa manufaa ya pande mbili katika zama mpya. Rais wa China amebainisha haya katika ukumbu mkuu wa watu wa China mjini Beijing.
Katika mazungumzo hayo,Rais wa China ameashiria pia vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, na kumweleza mwenzake wa Russia kwamba mzozo wa Asia ya Magharibi ulikuwa tete na kwamba kusitishwa vita ni suala la dharura.
Ameongeza: “Kusitishwa mapigano ni jambo la dharura kikamilifu, kuanzishwa tena mzozo ni jambo lisilofaa kabisa, na kwamba kuna umuhimu wa kipekee kuendelezwa mazungumzo katika uwanja huo.
Katika mazungumzo hayo, Rais Vladimir Putin wa Russia amesema: Dunia ya leo inahitaji ushirikiano wa dhati kati ya Russia na China.
Rais wa Russia pia amemtaja mwenzake wa China kuwa “rafiki mpendwa” na kwamba: “Ushirikiano kati ya Moscow na Beijing katika sera za kigeni ni moja ya mambo makuu ya kuleta utulivu katika uga wa kimataifa.”
