Iran: UNSC Iivunje ukimya kuhusu vitisho vya Marekani na uhalifu wa kivitaIran: UNSC Iivunje ukimya kuhusu vitisho vya Marekani na uhalifu wa kivita

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amelitaka Baraza la Usalama livunje ukimya wake kuhusu vitisho vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na ukiukaji wa kimfumo wa sheria za kimataifa za kibinadamu uliofanyika wakati wa vita haramu vya hivi karibuni.

Amir‑Saeid Iravani alitoa kauli hiyo siku ya Jumatano katika taarifa iliyowasilishwa mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa mdahalo wa wazi kuhusu “Ulinzi wa Raia”.

Alieleza masikitiko yake juu ya kushindwa kwa Baraza la Usalama kutekeleza wajibu wake mbele ya uhalifu wa kivita uliofanywa na Marekani na utawala wa Israel wakati wa mashambulizi yao ya kijeshi yasiyo na uhalali dhidi ya Iran.

Pia aliwashutumu watawala wavamizi kwa kulenga kwa makusudi raia pamoja na miundombinu ya kiraia, ikiwemo shule ya msingi katika mji wa kusini wa Minab, jambo lililosababisha kuuawa kwa zaidi ya wanafunzi wasio na hatia 168 pamoja na wafanyakazi wa shule hiyo.

Mjumbe huyo aliongeza: “Baraza la Usalama halipaswi kubaki kimya au kutojali vitisho vinavyotolewa mara kwa mara na kila siku na Rais wa Marekani dhidi ya Iran, vikiwemo vitisho vya wazi vya kuishambulia Iran kwa mabomu ‘hadi kurudishwa kwenye Enzi ya Mawe’, kuharibu miundombinu ya nishati, uchumi na viwanda ya nchi, kulenga wanasayansi wa nyuklia wa Iran na maafisa wa ngazi za juu, na hata matamshi yanayodokeza kuangamizwa kwa ustaarabu wa Iran.”

Amesema: “Kufanywa jambo la kawaida kwa vitisho hivyo vya matumizi ya nguvu, vitendo vya uchokozi, na matamshi ya uchochezi kutoka kwa mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama kunaweka mfano hatari.”

Wakati huohuo, Iravani amesema kuwa Marekani na utawala wa Israel, pamoja na wale wote waliowasaidia wavamizi hao na kurahisisha uvamizi wao, wanapaswa kubeba wajibu kamili wa kisheria na wa kimataifa kwa uhalifu wao mbaya dhidi ya taifa la Iran.

Aidha, mjumbe huyo ameitaka amesisitiza  kuwa hatua halali zilizochukuliwa na Iran wakati wa vita zilikuwa sambamba na haki ya kisheria ya kujilinda, akipinga majaribio ya kupotosha uhalisia wa hali halisi kama madai yasiyo na msingi na yenye msukumo wa kisiasa.

Vita vya kichokozi vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, vilianza tarehe 28 Februari kwa mashambulizi ya anga yaliyosababisha kuuawa raia wa kawaida wakiwemo watoto wa shule, maafisa wakuu wa Iran na makamanda wa ngazi za juu.

Vikosi vya ulinzi vya Iran vilijibu kwa kuanzisha mawimbi 100 ya mashambulizi ya kulipiza, yalikuwa yenye mafanikio, yakilenga shabaha nyeti na za kimkakati za Marekani na Israel kote katika eneo. Marekani ililazimika kutangaza usitishaji vita baada ya siku 40. Baada ya hapo mazungumzo ya kupitia upatanishi wa Pakistan yamekuwa yakiendelea bila mafanikio kutokana na ukaidi wa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *