Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yakemea mpango wa ‘Somaliland’ kufungua ubalozi katika al-Quds inayokaliwa kwa mabavuJumuiya ya Nchi za Kiarabu yakemea mpango wa ‘Somaliland’ kufungua ubalozi katika al-Quds inayokaliwa kwa mabavu

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) imekosoa vikali uamuzi wa eneo la Somaliland lililojitenga na Somalia wa kufungua ubalozi katika mji mtakatifu wa al Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel, ikisema hatua hiyo “haikubaliki kabisa.”

Katika taarifa, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Ahmed Aboul Gheit, amelaani kwa maneno makali uamuzi huo, akisema ni hatua iliyokataliwa na inayochochea hisia kali miongoni mwa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu.

Kiongozi huyo wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu pia ameonya kuhusu kuongezeka kwa ushawishi na upenyezaji wa Israel katika Ukanda wa Pembe ya Afrika.

Balozi wa eneo Somaliland lililojitenga na Somalia katika utawala haramu wa Israel alitangaza katika taarifa Jumatano kuwa eneo hilo lenye idadi kubwa ya Waislamu linatarajia kufungua hivi karibuni uwakilishi wa kidiplomasia katika al‑Quds.

Katika taarifa Jumatano serikali ya Somali imelaani vikali hatua ya eneo la Somaliland kufungua eti ubalozi huko Al Quds ni kinyume cha sheria zote za kimataifa.

Mnamo Desemba 2025, Israel ilitangaza kuitambua rasmi Somaliland kama eneo huru, hatua iliyokosolewa vikali duniani kote.

Serikali ya Shirikisho ya Somalia ilikataa vikali uamuzi huo, ikiutaja kuwa kinyume cha sheria za kimataifa na kusisitiza kwamba Somaliland bado ni sehemu isiyotenganishwa ya ardhi yenye mamlaka ya Jamhuri ya Somalia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *