Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imehitimisha mafunzo ya elimu ya uraia, utawala bora pamoja na ulinzi na usimamizi wa mali na rasilimali asilia yaliyokuwa yakitolewa kwa viongozi mbalimbali katika mkoa wa Shinyanga.
Mafunzo hayo yamewafikia viongozi kutoka Halmashauri zote sita za mkoa huo zikiwemo Kamati za Usalama, Sekretariet za Mkoa, Menejimenti za Halmashauri, Maafisa Madini, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata pamoja na Watendaji wa Vijiji na Mitaa.
Kupitia mafunzo hayo viongozi wamepata elimu kuhusu uwajibikaji, uzalendo, utawala bora na usimamizi sahihi wa rasilimali za taifa kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha, Serikali imeendelea kupongezwa kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo washiriki wamesema yameongeza uelewa na kuwajengea uwezo wa kuwahudumia wananchi kwa kuzingatia sheria na misingi ya utawala bora na kuiomba serikali mafunzo hayo yawe endelevu.
(Feed generated with FetchRSS)
