Wadau watahadharisha athari sintofahamu SUK ZanzibarWadau watahadharisha athari sintofahamu SUK Zanzibar

Dar es Salaam. Miezi sita baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, mvutano kuhusu uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) umeendelea kutawala siasa za Zanzibar, huku wadau wakionya hali hiyo inaweza kufufua migogoro ya kisiasa iliyowahi kugawa wananchi wa visiwani humo kwa miaka mingi.

Licha ya Katiba ya Zanzibar kuelekeza kuundwa kwa Serikali hiyo kwa kushirikisha vyama vilivyopata asilimia zinazostahili, hadi sasa chama cha ACT Wazalendo hakijaingia serikalini, jambo linaloibua maswali kuhusu mustakabali wa mfumo wa maridhiano ulioanzishwa mwaka 2010.

Wachambuzi wa siasa wanaeleza kuwa kuchelewa kwa makubaliano kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na ACT Wazalendo kunazidi kuongeza taharuki ya kisiasa, huku kila upande ukiendelea kusimamia masharti yake katika mazungumzo ya kuunda SUK.

ACT Wazalendo inasisitiza kuwa ushiriki wake serikalini haupaswi kuishia kwenye nafasi za juu za uongozi pekee, bali unapaswa kugusa pia ngazi za watendaji wa mikoa na wilaya, huku ikitaka kuwepo kwa maridhiano ya kweli yatakayoshughulikia chanzo cha migogoro ya kisiasa Zanzibar.

Kwa sasa, kamati ya CCM na ile ya ACT Wazalendo, zinaendelea na vikao kutengeneza makubaliano na kisha kutoka na tamko la pamoja na hatimaye kuunda SUK.

Kiini cha mvutano

Akizungumza kwa nyakati tofauti, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, husisitiza kuwa Serikali na CCM vinautambua umuhimu wa SUK na kwamba mazungumzo bado yanaendelea ili kuhakikisha mfumo huo unaendelea kama Katiba ya Zanzibar inavyoelekeza.

Lakini kwa upande wa ACT Wazalendo, msimamo umeendelea kuwa mgumu, hali inayoendeleza mvutano.

Kiongozi mkuu wa chama hicho, Dorothy Semu, anasema chama hicho hakiko tayari kuingia SUK kwa ajili ya kugawana nafasi za uongozi bila kuwepo kwa maridhiano ya kweli yatakayomaliza mivutano ya kisiasa inayoibuka mara kwa mara.

“Sisi hatuingii SUK kufuata vyeo, tunasimamia misingi ya kuanzishwa kwa SUK ambayo ililenga kumaliza matatizo ya Wazanzibari ya mikwamo ya kisiasa je, matatizo hayo yamekwisha? Tunataka umoja wa kitaifa wa kweli serikalini utakaowanufaisha wananchi na kumaliza tofauti ambazo zimekuwa zikiibuka mara kwa mara,” anasema.

Mbali na hilo, Semu anasema chama hicho kinataka uwajibikaji wa vitendo kwa waliohusika na mauaji ya raia yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, akisisitiza kuwa bila hatua za haki na uwajibikaji, chama hicho hakiwezi kuingia kwenye ushirikiano ambao hautatatua kiini cha migogoro ya kisiasa Zanzibar.

Kupitia maridhiano kati ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa zamani wa Civic United Front (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, Zanzibar ikaingia katika mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa uliolenga kuleta ushirikiano wa kisiasa badala ya ushindani wenye migawanyiko.

Licha ya mfumo huo kuonekana kuleta utulivu kwa kipindi fulani, migogoro iliendelea kujitokeza mara kwa mara.

Mwaka 2015, CUF ilikaa nje ya SUK baada ya kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika kufuatia kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar, hatua iliyozua mivutano mipya ya kisiasa na kuibua maswali kuhusu uimara wa mfumo huo wa maridhiano.

“Tunaikataa kabisa kura ya mapema, ambayo imeendelea kuchochea utata na migogoro wakati wa uchaguzi wa Zanzibar, haya ndiyo mambo tunayotaka yashughulikiwe ili tuingie SUK tukiwa na ushirikiano wa kweli wenye manufaa kwa jamii,” anasema Semu.

Athari kwa jamii

Mtaalamu wa masuala ya utumishi wa umma, siasa na utawala, Deus Kibamba anatahadharisha kuwa kusuasua kwa SUK kunaweza kuongeza kiwango cha kutokuaminiana kati ya wananchi, Serikali na upinzani.

“SUK inataka kuaminiana, mkiwa pamoja kwenye Baraza la Wawakilishi, mnatunga sera pamoja kiwango cha kuaminiana kitaongezeka,” anasema.

Anaonya kuwa kuendelea kwa mivutano hii kunaweza kuibua mpasuko wa kuaminiana katika jamii ya Zanzibar na hivyo kuathiri siasa zake.

Hata hivyo, anasema kwa mujibu wa sayansi ya siasa, Serikali inaweza kuendelea kufanya kazi hata kama baadhi ya nafasi za SUK bado hazijajazwa.

“Kulegalega kwa SUK hakuwezi kuwa sababu ya kulegalega kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. SUK ilianzishwa siyo kuongeza utendaji serikalini bali kuongeza kuaminiana kwa Serikali, upinzani na wananchi,” anasema.

Kibamba, anasema mifumo ya SUK imewahi kutumika katika mataifa mengine kama Zimbabwe kati ya Robert Mugabe na Morgan Tsvangirai pamoja na Kenya baada ya mgogoro wa uchaguzi uliowakutanisha Mwai Kibaki na Raila Odinga.

Kwa upande wake, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Utumishi, Laurean Ndumbaro anasema kutokuwepo kwa mawaziri kutoka ACT Wazalendo hakuwezi kuathiri kwa kiwango kikubwa utendaji wa Serikali kwa sababu mfumo wa Serikali unaendelea kupitia makatibu wakuu na watendaji wengine wa umma.

“Hata Makamu wa Kwanza wa Rais bado hajapatikana, lakini uendeshaji wa shughuli za Serikali bado unaweza kuendelea kama kawaida bila athari kubwa. Shida hapa inabaki ileile kuwa uwakilishi wa upinzani unakosekana,” anasema.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dk Anna Henga, anasema kuchelewa kukamilika kwa SUK kunakiuka haki ya kikatiba inayotaka Serikali hiyo kuundwa ndani ya siku 90 baada ya uchaguzi.

“Kuendelea kwa mvutano huu kunasababisha ombwe la uongozi Zanzibar kwani bado kuna nafasi muhimu serikalini zinaendelea kubaki wazi.”

“Haki iliyocheleweshwa ni haki iliyokiukwa, hivyo wafanye haraka wamalize tofauti zao wakubaliane Serikali ikamilike wananchi wapate haki zao za uwakilishi ipasavyo,” anasema.

Suluhisho la kudumu

Wakati mvutano huo ukiendelea, wachambuzi wa siasa wanaonya kuwa mustakabali wa SUK sasa unategemea zaidi utashi wa kisiasa kuliko sheria.

Wakili Alloyce Komba anasema kauli kali zinazoendelea kutolewa na pande za maridhiano hayo zinaashiria kupungua kwa mazingira ya maelewano.

“Tatizo linalofanya migogoro ya SUK kuwa endelevu ni ukosefu wa utashi wa kisiasa. Ukiangalia matamko ya viongozi yamekuwa makali yasiyoashiria nia njema ya maridhiano yatakayowezesha kufikiwa kwa uundwaji wa SUK,” anasema.

Komba anasisitiza kuwa iwapo pande zinazotakiwa kupeleka majina ya viongozi wa kuingia kwenye SUK hazitafikia mwafaka, hakuna upande utakaonufaika na hali hiyo, akisisitiza umuhimu wa kukubaliana.

 “Hiki ni kitu ambacho siyo kizuri. Rais Mwinyi anafanya vizuri kwenye uchumi, ujenzi wa barabara lakini kisiasa hili la SUK linaweza kuchafua awamu hii ya uongozi wake, hasa kwa siasa za Zanzibar. Suluhu hapa ni utashi wa kisiasa tu,” anasema.

Miezi sita tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 mvutano wa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) umeendelea kutikisa siasa za Zanzibar, hali ambayo wadau wanasema inatishia kufufua mgogoro wa kisiasa visiwani humo.

Wadau hao wa siasa, wamesema mwendelezo wa hali hiyo isiyofika mwisho, huenda ikafufua kumbukumbu za migogoro ya kisiasa iliyowahi kuwagawa Wazanzibari kwa miaka mingi kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo mwaka 2010.

Mitazamo hiyo inaibuka, ikiwa imepita miezi sita tangu Zanzibar iunde Serikali, lakini hadi sasa bado ACT Wazalendo iliyokuwa na zaidi ya asilimia 20 ya kura katika uchaguzi huo, haijaingia ndani ya Serikali.

Kusuasua kwa hatua hiyo, kunatokana na kila upande kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na ACT Wazalendo, kuweka masharti yake ili kufanikisha hilo. ACT Wazalendo inataka Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), isihusishe nafasi za juu pekee, bali ifike hadi kwa watendaji ndani ya mikoa na wilaya.

Kwa sasa, kamati ya CCM na ile ya ACT Wazalendo, zinaendelea na vikao kutengeneza makubaliano na kisha kutoka na tamko la pamoja na hatimaye kuunda SUK.

Kiini cha mvutano

Akizungumza kwa nyakati tofauti, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza Serikali na CCM vinautambua umuhimu wa SUK na kwamba mazungumzo bado yanaendelea ili kuhakikisha mfumo huo unaendelea kama Katiba ya Zanzibar inavyoelekeza.

Lakini kwa upande wa ACT Wazalendo, msimamo umeendelea kuwa mgumu, hali inayoendeleza mvutano.

Kiongozi mkuu wa chama hicho, Dorothy Semu, amesema chama hicho hakiko tayari kuingia SUK kwa ajili ya kugawana nafasi za uongozi bila kuwepo kwa maridhiano ya kweli yatakayomaliza mivutano ya kisiasa inayoibuka mara kwa mara.

“Sisi hatuingii SUK kufuata vyeo, tunasimamia misingi ya kuanzishwa kwa SUK ambayo ililenga kumaliza matatizo ya Wazanzibari ya mikwamo ya kisiasa, je matatizo hayo yamekwisha?. Tunataka umoja wa kitaifa wa kweli serikalini utakaowanufaisha wananchi na kumaliza tofauti ambazo zimekuwa zikiibuka mara kwa mara,” amesema.

Mbali na hilo, Semu amesema chama hicho kinataka uwajibikaji wa vitendo kwa waliohusika na mauaji ya raia yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, akisisitiza kuwa bila hatua za haki na uwajibikaji, chama hicho hakiwezi kuingia kwenye ushirikiano ambao hautatatua kiini cha migogoro ya kisiasa Zanzibar.

Kupitia maridhiano kati ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa zamani wa Civic United Front (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, Zanzibar ikaingia katika mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa uliolenga kuleta ushirikiano wa kisiasa badala ya ushindani wenye migawanyiko.

Licha ya mfumo huo kuonekana kuleta utulivu kwa kipindi fulani, migogoro iliendelea kujitokeza mara kwa mara.

Mwaka 2015, CUF ilikaa nje ya SUK baada ya kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika kufuatia kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar, hatua iliyozua mivutano mipya ya kisiasa na kuibua maswali kuhusu uimara wa mfumo huo wa maridhiano.

“Tunaikataa kabisa kura ya mapema, ambayo imeendelea kuchochea utata na migogoro wakati wa uchaguzi wa Zanzibar, haya ndiyo mambo tunayotaka yashughulikiwe ili tuingie SUK tukiwa na ushirikiano wa kweli wenye manufaa kwa jamii,” anasema Semu.

Athari kwa jamii

Mtaalamu wa masuala ya utumishi wa umma, siasa na utawala, Deus Kibamba anatahadharisha kuwa kusuasua kwa SUK kunaweza kuongeza kiwango cha kutokuaminiana kati ya wananchi, Serikali na upinzani.

“SUK inataka kuaminiana, mkiwa pamoja kwenye Baraza la Wawakilishi, mnatunga sera pamoja kiwango cha kuaminiana kitaongezeka,” amesema.

Anaonya kuwa kuendelea kwa mivutano hii kunaweza kuibua mpasuko wa kuaminiana katika jamii ya Zanzibar na hivyo kuathiri siasa zake.

Hata hivyo, anasema kwa mujibu wa sayansi ya siasa, Serikali inaweza kuendelea kufanya kazi hata kama baadhi ya nafasi za SUK bado hazijajazwa.

“Kulegalega kwa SUK hakuwezi kuwa sababu ya kulegalega kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. SUK ilianzishwa siyo kuongeza utendaji serikalini bali kuongeza kuaminiana kwa Serikali, upinzani na wananchi,” amesema.

Kibamba, anasema mifumo ya SUK imewahi kutumika katika mataifa mengine kama Zimbabwe kati ya Robert Mugabe na Morgan Tsvangirai pamoja na Kenya baada ya mgogoro wa uchaguzi uliowakutanisha Mwai Kibaki na Raila Odinga.

Kwa upande wake, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Utumishi, Laurean Ndumbaro amesema kutokuwepo kwa mawaziri kutoka ACT Wazalendo hakuwezi kuathiri kwa kiwango kikubwa utendaji wa Serikali kwa sababu mfumo wa Serikali unaendelea kupitia makatibu wakuu na watendaji wengine wa umma.

“Hata Makamu wa Kwanza wa Rais bado hajapatikana, lakini uendeshaji wa shughuli za Serikali bado unaweza kuendelea kama kawaida bila athari kubwa. Shida hapa inabaki ileile kuwa uwakilishi wa upinzani unakosekana,” amesema.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dk Anna Henga, anasma kuchelewa kukamilika kwa SUK kunakiuka haki ya kikatiba inayotaka Serikali hiyo kuundwa ndani ya siku 90 baada ya uchaguzi.

“Kuendelea kwa mvutano huu kunasababisha ombwe la uongozi Zanzibar kwani bado kuna nafasi muhimu serikalini zinaendelea kubaki wazi.

“Haki iliyocheleweshwa ni haki iliyokiukwa, hivyo wafanye haraka wamalize tofauti zao wakubaliane Serikali ikamilike wananchi wapate haki zao za uwakilishi ipasavyo,” amesema.

Suluhisho la kudumu

Wakati mvutano huo ukiendelea, wachambuzi wa siasa wanaonya kuwa mustakabali wa SUK sasa unategemea zaidi utashi wa kisiasa kuliko sheria.

Wakili Alloyce Komba anasema kauli kali zinazoendelea kutolewa na pande za maridhiano hayo zinaashiria kupungua kwa mazingira ya maelewano.

“Tatizo linalofanya migogoro ya SUK kuwa endelevu ni ukosefu wa utashi wa kisiasa. Ukiangalia matamko ya viongozi yamekuwa makali yasiyoashiria nia njema ya maridhiano yatakayowezesha kufikiwa kwa uundwaji wa SUK,” amesema.

Komba anasisitiza kuwa iwapo pande zinazotakiwa kupeleka majina ya viongozi wa kuingia kwenye SUK hazitafikia mwafaka, hakuna upande utakaonufaika na hali hiyo, akisisitiza umuhimu wa kukubaliana.

 “Hiki ni kitu ambacho siyo kizuri. Rais Mwinyi anafanya vizuri kwenye uchumi, ujenzi wa barabara lakini kisiasa hili la SUK linaweza kuchafua awamu hii ya uongozi wake, hasa kwa siasa za Zanzibar. Suluhu hapa ni utashi wa kisiasa tu,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *