Je, Benin na Niger zinaelekea kufufua mahusiano baada ya Benin kupata rais mpyaJe, Benin na Niger zinaelekea kufufua mahusiano baada ya Benin kupata rais mpya

Ujumbe wa Niger, ukiongozwa na Waziri Mkuu, ulikuwepo katika sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya wa Benin mnamo Mei 24, 2026. Je, hii ni ishara ya kuanzishwa kwa uhusiano kati ya nchi mbili ambazo zimekuwa na mvutano tangu mapinduzi ya Julai 26, 2026, nchini Niger?

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Je, uhusiano kati ya Benin na Niger uko katika hatua ya mwanzo ya  kuanzishwa kwake? Umekuwa mgumu kati ya majirani hao wawili tangu mapinduzi ya Niger mnamo Julai 2023. Mpaka bado umefungwa upande wa Niger.

Je, kuwasili kwa rais mpya nchini Benin kunaweza kupunguza mvutano? Romuald Wadagni aliapishwa Mei 24, 2026. Na ujumbe wa Niger, ukiongozwa na Waziri Mkuu Ali Mahamane Lamine Zeine, ulishiriki katika sherehe hiyo. 

Ujumbe wa Niger wakaribishwa kwa vifijo na nderemo

Ujumbe wa Niger ukiongozwa na Waziri Mkuu wa Niger, Ali Mahamane Lamine Zeine, ambaye aliambatana na mawaziri wawili, akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani Mohamed Toumba ulikaribishwa na vifijo na nderemo. “Ninaamini hii ni njia mpya inayofunguka. Jambo muhimu zaidi ni kufanya kazi kuelekea kuimarisha uhusiano,” aliwaambia waandishi wa habari.

Waangalizi wanajiuliza kama mabadiliko ya uongozi wa Benin na kuondoka kwa Patrice Talon, ambaye alikuwa kitovu cha mvutano na nchi jirani ya Niger, kunaweza kusababisha kuazishwa tena kwa uhusiano. Majaribio ya awali yalishindwa.

Suala hili ni miongoni mwa mambo yatakayoshughulikiwa na rais mpya wa Benin, ambaye aliliweka kipaumbele katika hotuba yake ya kuapishwa. “Katika eneo hili linalokabiliwa na tishio la ugaidi, tunalazimika kufanya kazi pamoja,” Romuald Wadagni alibainisha.

Soma piaBenin: Baada ya kuapishwa, rais mteule Romuald Wadagni ateua serikali yake

Matarajio ni makubwa pande zote mbili za mpaka ambao umefungwa kwa karibu miaka mitatu, na kuathiri usafiri wa watu na usafirishaji wa bidhaa, ingawa bandari ya Cotonou ilikuwa njia rahisi zaidi ya kufika kutoka Niger.

“Kila mtu alithamini ziara hiyo”

Gamatié Mahamadou, Katibu Mkuu wa Muungano wa vyama vya Uchukuzi na Wafanyakazi nchini Niger (UTTAN), anatumai kuanza tena kwa majadiliano kati ya mamlaka za nchi hizo mbili, kwa lengo la kufungua tena mpaka. “Pande zote mbili, kila mtu alithamini ziara ya ujumbe,” alimwambia Magali Lagrange. “Watu wana matumaini kwamba, kwa timu mpya ya serikali nchini Benin, mazungumzo yanaweza kusonga mbele, kwa sababu mgogoro huu haufaidii mtu yeyote. Katika historia ya uhusiano kati ya Niger na Benin, kwa ufahamu wangu, hatujawahi kuwa na mgogoro kama huo, kutokana na kufungwa kwa mpaka huu.”

Huko Niamey, uteuzi wa Gildas Agonkan katika serikali ya Benin pia ulibainika. Balozi wa zamani wa Benin nchini Niger alichukua nafasi ya Waziri wa Ulinzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *