Moscow inatoa wito kwa wakazi wa Kyiv kuondoka kabla ya mashambuliziMoscow inatoa wito kwa wakazi wa Kyiv kuondoka kabla ya mashambulizi

Diplomasia ya Urusi siku ya Jumatatu imewataka raia wa kigeni wanaoishi Kyiv, wakiwemo wafanyakazi wa kidiplomasia, kuondoka katika mji mkuu wa Ukraine kabla ya mashambulizi zaidi ya anga ya Urusi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili linakuja baada ya mashambulizi makubwa ya anga ya Urusi kuilenga Ukraine mwishoni mwa wiki hii iliyopita, ikiwa ni pamoja na Kyiv, na kuua watu wasiopungua wanne na kuwajeruhi takriban 100. Urusi ilirusha kombora la kisasa la Oreshnik kwa mara ya tatu tangu kuanza kwa mzozo huo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imeonya katika taarifa, bila kutaja muda maalum wa mashambulizi hayo kwamba “mashambulizi mapya yatafanyika katika vituo vya kufanya maamuzi” na “makampuni makubwa ya kijeshi”. “Tunawashauri raia wa kigeni, wakiwemo wafanyakazi wa misheni za kidiplomasia na mashirika ya kimataifa, kuondoka jijini haraka iwezekanavyo, na kuwashauri wakazi wa mji mkuu wa Ukraine kujiepusha na miundombinu ya kijeshi na kiutawala,” taarifa hiyo iliongeza.

“Msikubali kusalitiwa na Urusi”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andriy Sybiga amewataka washirika wa Kyiv “wasikubali kusalitiwa na Urusi” na watoe misaada na silaha zaidi kwa Ukraine. Ufaransa, kwa upande wake, imepuuza onyo la Urusi. “Tumezoea vitisho vya Putin. Kuwaondoa wanadiplomasia wetu ni jambo lisilowezekana,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesema ilipoulizwa na waandishi wa habari.

Licha ya onyo hili kuhusu Kyiv, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ambaye kwa sasa anazuru India, amebainisha leo Jumanne kwamba “Marekani iko tayari kwa lolote na iko tayari kufanya kila kitu kwa uwezo wake kuwezesha kusitishwa kwa vita hivi,na tunatumaini kwamba fursa hiyo itahuhudiwa wakati fulani.”

Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump umekuwa ukijaribu kukomesha mapigano kwa kuandaa nduru mbalimbali za mazungumzo kati ya pande hizo mbili huko Abu Dhabi, na pia huko Geneva mwezi Februari. Hata hivyo, mazungumzo ya pande tatu yamesitishwa tangu kuzuka kwa vita Mashariki ya Kati mnamo Februari 28, ingawa Moscow na Kyiv zote zinasema ziko tayari kuyaanzisha tena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *