Tanzania imeandika historia mpya katika sekta ya afya baada ya Dkt. Livin Peter Mumburi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kufaulu kuwa daktari bingwa wa magonjwa wa mfumo wa chakula na ini kwa watoto, baada ya kuhitimu mafunzo maalum nchini Afrika Kusini.
Dkt. Mumburi anakuwa daktari wa kwanza na pekee nchini Tanzania mwenye utaalamu huo, baada ya kukamilisha mafunzo ya uzamivu wa kimatibabu ya miaka miwili katika Chuo Kikuu cha Cape Town, hatua inayotajwa kufungua ukurasa mpya wa huduma za kibingwa za mfumo wa chakula na ini kwa watoto hapa nchini.
Akizungumza baada ya kurejea nchini, Dkt. Mumburi ameeleza kuwa changamoto za magonjwa ya ini na mfumo wa chakula kwa watoto bado ni kubwa Tanzania, huku akisisitiza kuwa watoto wengi wanahitaji huduma za kibingwa zinazopatikana kwa uchache.
(Feed generated with FetchRSS)
