
Watu zaidi ya 30 wameuawa kufuatia mashambulizi mapya ya jeshi la Israeli, Kusini na Mashariki mwa nchi ya Lebanon, baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, kuagiza operesheni ya kijeshi dhidi ya kundi la Hezbollah.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wizara ya afya nchini Lebabon, inasema miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni watoto.
Jeshi la Israeli linasema katika mashambulizi hayo, imefanikiwa kuharibu miundo mbinu na ngome zaidi ya 100 ya kundi ya Hezbollah, katika mashambulizi mazito kuwahi kutekelezwa tangu mwezi Aprili.
Netanyahu amesema mashambulizi hayana yanalenga pia kuwalinda Waisraeli, waishio Kaskazini mwa nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kundi la Hezbollah.
Haya yamejiri licha ya kuwepo kwa mkataba kati ya Israel na Lebanon, lakini umeendelea kukiukwa mara kwa mara kufuatia kuendelea kwa mashambulizi kati ya pande zote.
Wakati hayo yakijiri, maafisa nchini Iran, wameishtumu Marekani kwa kukiuka makubaliano ya usitishwaji vita, baada ya wanajeshi wake kutekeleza mashambulizi karibu na eneo la Bahari la mlango wa Hormuz. Washington inasema mashambulizi hayo yalitekelezwa ili kujilinda.
