Kenya: Wanafunzi 16 wafariki kwenye mkasa wa moto katika bweni laoKenya: Wanafunzi 16 wafariki kwenye mkasa wa moto katika bweni lao

Mamlaka nchini Kenya imethibitisha kufariki kwa wanafunzi 16 kwenye mkasa wa moto kwenye bweni lao, wengine 79 wakiripotiwa kujeruhiwa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Inaelezwa kuwa moto huo ulianza saa saba usiku kwa saa Nairobi kwenye shule ya Wasichana ya Utumishi katika kaunti ya Nakuru, karibia Kilomita 120 kutoka jijini Nairobi.

Kwa mujibu wa mamlaka, shule hiyo ilikuwa na wanafunzi 808 wakati wa mkasa huo, wanafunzi 7 wakiripotiwa kulazwa hospitalini.

Wanafunzi karibia 200 walikuwa kwenye bweni hilo ambalo limeteketea kwa mujibu wa mamlaka.
Wanafunzi karibia 200 walikuwa kwenye bweni hilo ambalo limeteketea kwa mujibu wa mamlaka. REUTERS – Thomas Mukoya

Wazazi wa wanafunzi wanaosoma kwenye shule hiyo wamewasili shuleni kutaka kujua hali ya watoto wao. Hadi tukichapisha taarifa hii, chanzo cha moto huo hakikuwa kimewekwa wazi.

Visa vya moto kwenye shule vimekuwa vikiripotiwa katika shule kadhaa nchini Kenya, serikali ikiagiza baadhi ya mabadiliko kufanywa kwenye miundombinu ya shule za kutwa kwa ajili ya usalama wa wanafunzi.

Wazazi waliofika kwenye shule hiyo kutaka kufahamu hali ya wanao.
Wazazi waliofika kwenye shule hiyo kutaka kufahamu hali ya wanao. REUTERS – Monica Mwangi

Mwaka wa 2024, moto kwenye shule ya Hillside Endarasha katika kaunti ya Nyeri kwenye mkoa wa kati ulisababisha vifo vya wanafunzi 21 wa kiume.

Katika baadhi ya matukio, wanafunzi walituhumiwa kuteketeza shule zao wenyewe. Mwaka wa 2018 visa 63 vya wanafunzi kuteketeza shule viliripotiwa.

Kufuatia matukio hayo ya mwaka wa 2024, serikali ya Kenya iliahidi kufanyia shule kadhaa ukaguzi kuhakikisha usalama wa wanafunzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *