
Nchini Mali, jeshi limeendelea kutekeleza mashambulizi dhidi ya kundi la waasi wa Azawad Liberation Front wanaoshirikiana na wanajihadi katika mji wa Kidal, Kaskaeini mwa nchi hiyo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Msikiti mkubwa mjini Kidal na nyumba kadhaa, ikiwemo ile ya Bilal Ag Achérif, rais wa waasi wa FLA, ilishambuliwa na kuharibiwa siku ya Jumatano.
Jeshi limeendeleza mashambulizi haya baada ya waasi hao wanaoshirikiana na wanajihadi wa JNIM kutekeleza mashambulio makubwa katika maeneo mbalimbali ya Mali, na kudhibiti mji wa Kidal.
Mbali na mashambulizi hayo makundi hayo yenye silaha, yamesonga mbele na kudhibiti mji mwingine wa Tessalit tangu tarehe moja mwezi Mei.
Haya yanajiri wakati huu wanajeshi wa Mali wakisalia tu kwenye kambi mbili za Aguelhoc na Anefis, ambazo pia zina mamluki kutoka Urusi, huku mapambano ya udhibibiti wa mji wa Kidali, yakiendelea.
