Shirika la afya duniani limesema mzozo unaoshuhudiwa nchini Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo, unalemaza juhudi za kukabiliana na mlipuko mpya wa virusi hatari vya Ebola nchini humo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus kupitia mtandao wake wa X amelezea kuhofia athari ya vita vya Mashariki mwa nchi hiyo hali ambayo anasema inatishia kuleta mgongano wakiafya na kivita na kufanya kuwa vigumu kudhibiti ugonjwa huo.
Kulingana na Tedros, vita vinavyosababisha watu kuhama makzi yao vinatishia kuwafanya watu ambao huenda wameambukizwa kutangamana na watu wengine kwenye kambi zilizo na msongamano.
Hadi kufikia sasa shirika hilo la afya duniani limerekodi vifo 10 vilivyothibitishwa, na vifo 223 vinavyoshukiwa kusababishwa na virusi hivyo tangu mlipuko huo ulipotangazwa katikati ya mwezi huu wa Mei.
Haya yanajiri wakati nchi Jirani ya Uganda, ikithibitisha kifo kimoja kutokana na ugonjwa huo na visa sita vya maambukizo huku pia nchi hiyo ikitangaza kufunga mara moja mpaka wake na DRC, pamoja na kutangaza siku 21 ya kukaa karantini kwa yeyote anayewasili kutoka DRC.
